Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais Boubacar Diara wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Mali (FMF) kwa kutwaa Ubingwa wa Afrika kwa vijana U17.
Katika salam zake mh. Malinzi amesema mafanikio mazuri waliyoyapata FMF yametokana na uongozi bora, kamati ya utendaji na mipango thabiti waliyoiweka katika soka la Vijana.
Kwa kutwaa Ubingwa wa vijana Afrika U17, Mali wamepata nafasi ya kuliwakilisha Bara la Afrika kwenye fainali za U17 za Dunia nchini Chile pamoja na nchi za Afrika Kusini,Guinea na Nigeria.
Mali wametwaa Ubingwa wa vijana Afrika U17 baada ya kuifunga timu ya taifa ya vijana ya Afrika Kusini (Amajimbo's) kwa mabao 2-0.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), watanzania wanawapa pongezi Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Mali (FMF) wa kutwaa Ubingwa huo.
Aidha Rais Malizi pia ametuma salam za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Afrika Kusini (SAFA) Bw. Dany Jordaan kwa timu ya Amajimbo's kushika nafasi ya pili.
Amajimbo's ndio timu pekee kusini mwa Bara la Afrika watakaowaklisha kwenye fainali za U17 za Dunia nchini Chile.
BEACH SOCCER YAENDELEA KUJIFUA BAMBA BEACH
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Sola la Ufukweni (Beach Soccer) iliyoingia kambini mwishoni mwa wiki Bamba Beach Kigamboni, inaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya timu ya Taifa Soka la Ufukweni ya Misri mwishoni wiki ijayo.
Maandalizi ya mchezo dhidi ya timu ya Misri yanaendelea vizuri Bamba Beach Kigamboni chini ya kocha mkuu John Mwansasu ambaye aliingia kambini mwishoni mwa wiki na wachezaji 14.
Mchezo wa kwanza unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya Machi 13 katika klabu ya Escape 1 Msasani jijini Dar es salaam na marudio yake kufanyika baada ya wiki moja nchini Misri.
Tanzania ilifanikiwa kufuzu hatu ya pili baada ya kuitoa timu ya Taifa ya Kenya kwa jumla ya mabao 12- 9, mchezo wa awali Mombasa Tanzania ilishinda kwa mabao 5-3, na mchezo wa marudiano uliofanyika klabu ya Escape 1 kuibuka na ushindi wa mabao 7-6.
Fainali za Mataifa Afrika kwa Sola la Ufukweni (Beach Soccer) zinatarajiwa kufanyika mwezi April 2015 katika Visiwa vya Shelisheli.
VPL KUENDELEA JUMATANO
Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi katika viwanja vitatu tofauti siku ya jumatano, Mkoani Morogoro katika uwanja wa Manungu-Turiani timu ya Mtibwa Sugar watawaribisha majirani zao timu ya Polisi Morogoro.
Katika uwanja wa Azam Complex - Chamazi maafande wa JKT Ruvu watawakaribisha maafande wenzao timu ya Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya, huku timu ya Ruvu Shooting wakiwa katika Uwanja wa nyumbani Mabatini - Mlandizi kuwakaribisha timu ya Ndanda FC.
NB: Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom imeambatanishwa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment