Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex
Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu
taarifa za upotoshwaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na
Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Honoratha kilichopo Temeke jijini Dar es
Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex
Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu
taarifa za upotoshwaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na
Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Honoratha kilichopo Temeke jijini Dar es
Salaam.
NA LOVENESS BERNARD
MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotion,
Alex Msama, amesikitishwa na taarifa za upotoshaji zilizotolewa hivi karibuni
kuhusu kituo cha kulea watoto yatima cha Honoratha kilichopo wilayani Temeke
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, amesema kuwa Kituo hicho ni moja ya vituo anavyovihudumia kila mwezi na hakina
tatizo la kuwalaza watoto madarasani, kwani wana vyumba kwa ajili ya malazi na
kwamba, picha zilizoonyeshwa zilipigwa
watoto hao wakiwa darasani.
‘’Nimesikitishwa na taarifa hizi,
kwani Honoratha ni moja ya vituo ambavyo ninavihudumia, changamoto zao
nazifahamu...Kinalea watoto vizuri na baadhi yao wengine tunawasomesha vyuo vikuu
mbalimbali hapa nchini,” alisema Msama.
Aidha, Msama amevitaka vyombo vya
habari kuandika habari za ukweli na uhakika ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kwa wahusika, ikiwamo kwa
mlezi na watoto wanaoishi katika kituo hicho ambao walipata adha baada ya
taarifa hiyo kutoka.
Alisisitiza kuwa, taarifa hizo hazina
ukweli wowote kwani hata mlezi wa kituo hicho hawakufanya mahojiano naye,
ikiwamo kumuuliza kwa nini watoto hao walilala darasani mchana huo.
Msama amekuwa akisaidia vituo
mbalimbali vya kulea yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia vyanzo
vyake mbalimbali ikiwamo mapato yanayotokana na Tamasha la Pasaka.
No comments:
Post a Comment