MAMLAKA YA
WANANCHI 7-(1)
Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na kwa hiyo:
(a) Serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi ambao kwa umoja na ujumla wao wanamiliki na kuipatia Katiba hii uhalali.
(a) Serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi ambao kwa umoja na ujumla wao wanamiliki na kuipatia Katiba hii uhalali.
(b) Lengo kuu la
Serikali litakuwa ni maendeleo na ustawi wa wananchi.
(c)Serikali
itawajibika kwa wananchi.
(d)Wananchi watashiriki
katika shughuli za Serikali kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(2) Kwa mujibu wa
Ibara hii, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar zitapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi kupitia uchaguzi
wa kidemokrasia na utakaoendeshwa na kusimamiwa na vyombo vitakavyopewa mamlaka
na Katiba hii na Katiba ya Zanzibar, kwa kadri itakavyokuwa.
No comments:
Post a Comment