HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 28, 2015

Zaidi ya wanafunzi 60,000 wa UDOM kufurahia Airtel WI-FI


Dodoma, Aprili 28, 2015, Kufahamu ukweli kwamba Dodoma ni mji mteule na wenye kuendelea kwa kasi hapa nchini na mji uliobahatika kuwa miongoni mwa mji wenye chuo kikubwa hapa Tanzania, Airtel imeendelea na utamaduni wake wa kutoa huduma  iliyo bora kwa Watanzania.

Leo, Airtel Tanzania imezindua huduma yenye  ufanisi na gharama nafuu UNI WI-FI ambayo itawezesha wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma kupata huduma iliyo bora na nafuu, ambayo  itaweza kukidhi mahitaji  kwa wanafunzi wapatao zaidi ya 60,000 na wanachama wa taaluma mbalimbali yenye kasi kubwa na inayopatikana kwa bei nafuu.
Afisa masoko wa Airtel Tanzania, Prospa Mwanda akionyesha kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi Intaneti  inavyofanya kazi mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo chuoni hapo. Airtel Tanzania chuoni hupo imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu.
Meneja Masoko wa Airtel Uni Wi-Fi, Aneth Muga anaepiga picha ya selfie ili waitume kwa kutumia huduma ya Airtel Wi-Fi intaneti kwa baadhi ya uongozi wa wanafunzi na mshauri wa wanafunzi chuoni hapo mara baada ya Airtel kuzindua huduma yao ya  intaneti Wi-Fi yenye kasi zaidi  maalum kwa wanafunzi wa chuo hicho.

Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) bw, Dick Manong akiongea na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UNI Wi-Fi jana chuoni hapo ambapo itawasaidia wanafunzi kupata intaneti kwa gaharama nafuu ya yenye kasi zaidi.


No comments:

Post a Comment

Pages