CHAMA cha Wananchi
(CUF), Kata ya Kigogo wilayani Ilala Dar es salaam kimepiga kura ya maoni kwa ajili ya kupata
mgombea atakayeweza kupambanishwa na wagombea wengine Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa).
Vyama vinavyo unda
umoja huo ni Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), NLD na NCCR-Mageuzi.
Akizungumza na
wandishi wa habari kuhusu mchakato huo, Katibu Kata wa CUF Kata ya Kigogo,
Khalid Singano ambaye pia ni mgombea wa chama hicho, alisema wanachofanya ni
hatua ya awali.
Alisema baada ya
kura hiyo ya ndani mshindi atashindanishwa na wagombea wengine kutoaka vyama
vinavyounda umoja huo kwa ajili ya kumpata mshindi wa jumla atakayepambana na
yule Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Vigezo
vitakavyotumika kumpata mshindi huyo wa jumla, itaangaliwa takwimu za vyama
vyote zinazohusiana na chaguzi mbalimbali zilizopita, kukubalika kwa chama na
kukubalika kwa mgombea,”alisema Singano.
Singano, aliwataja
wagombea hao kuwa ni Mwinyi Madenge,
Baraka Nyakite, Iddi Maza, Sellemani Sellemani pamoja na yeye mwenyewe
(Singano).
Alisema upepo wa
kura hizo za ndani ulikuwa ukiangalia zaidi uwezo wa watendaji ambao wameweza
kukisaidia chama na kukifanya kipate mitaa mitatu katika uchaguzi wa serikali
za mitaa mwaka jana.
“Sio dhambi mimi ni
miongoni mwa watendaji wa chama hiki tuliyoshiriki katika kukiimarisha katika
kata hii ya kigogo kwa hiyo uwezo wa kuongoza kata ni nao,”alisema.
Hadi gazeti hili
linakwenda mitamboni matokeo yalikuwa bado hayajatangazwa.
No comments:
Post a Comment