NA ELIZABETH JOHN
MSANII wa filamu za Bongo, Kajala Masanja, amempa matumaini msanii mwenzie
ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu, Wema Sepetu kwamba bado ni binti mdogo na
asikate tamaa kwamba hatapa tena mtoto.
Kauli hiyo ya Kajala imekuja siku chache baada ya Wema kuweka wazi kwamba
daktari amemwambia hana uwezo wa kupata mtoto kitu ambacho kinamuumiza sana.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kajala alisema kuwa, licha ya
daktari kumthibitishia hivyo bado anauwezo wa kuendelea kutafuta madaktari
ambao wanauwezo wa kumtibu tatizo alilonalo.
"Wema bado binti mdogo, kama kweli ana nia ya kupata mtoto azidi
kuhangaika kwa madakaktari bingwa, kuna watu wanaishi ndani ya ndoa miaka mingi
bila mtoto lakini badae wanapata kikubwa asikate tamaa," alisema.
Kajala aliwataka wapenzi wa kazi zake kumpokea katika ujio wa filamu yake mpya
inayojulikana kwa jina la 'Pishu' ambayo imeingia sokoni hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment