Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk (wa tatu kulia), wengine ni wawakilishi kutoka balozi huo. (Picha zote na Loveness Bernard)
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa amebeba ndoo ya maji kichwani alipokuwa akikabidhiwa visima 33 vilivyochimbwa kwa msaada wa Watu wa Falme za Kiarabu na Balozi wa Falme hizo.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akifungua bomba la maji kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji katika Kata ya Olosokwani, Loliondo wilayani Ngorongoro, juzi. Mradi huo umefadhiliwa na Serikali ya Falme za Kiarabu (UAE) ambayo imewekeza wilayani humo. Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa UAE nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akijindaa kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kata ya Olosokwani, ambako alizindua mradi mkubwa wa maji ya visima virefu wilayani Ngorongoro, juzi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro,Hashimu Shaibu.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akifurahia jambo na wakazi wa kijiji Olosokwani, baada ya kuzindua mradi wa maji wa visima virefu wilayani Ngorongoro juzi. Kushoto ni Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk.

Na Loveness Bernard
Wafugaji kutoka nchi za jirani waliovamia katika eneo la Loliondo wametakiwa kuondoa mifugo yao mara moja ili
kuliacha eneo hilo kubaki na amani.
Akizungumza na wananchi na wafugaji wa kijiji cha
Ololosokwani, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema wakazi wa Loliondo
wanauwezo wa kutatua migogoro yao wenyewe ila wanaosababisha migogoro hiyo
isiishe na kuibuka mara kwa mara ni wageni wanaoingia katika eneo hilo na
kuchungia mifugo yao.
“Ninatoa tahadhali kwa wageni wanaoitazama loliondo kwa
jicho la husda waache kufugia mifugo yao loliondo, kila mmoja afugie kwao ardhi
ya loliondo ni ya wana loliondo na sio wageni” alisema Nyalandu.
Alisema changamoto kubwa inayoikabili eneo hilo la Loliondo ni
ongezeko la watu na mifugo wakati ardhi ikibaki kuwa ile ile.
Nyalandu alisema kuna haja ya kuendeleza uhifadhi ili eneo
la Loliondo liendelee kustawi na wageni waendelee kuja Loliondo ambapo
watachangia utalii endelevu katika shughuli kama za utalii wa picha na
uwindaji.
Akizungumzia kuhusu miradi ya maji aliyoikabidhi kwa
wananchi wa loliondo jana kutoka kwa Balozi wa Falme za Kiarabu waliofadhiri
ujenzi wa miradi hiyo iliyogharimu sh bilioni 1.6 Waziri Nyalandu alisema hayo
ni matunda ya ushirikiano mzuri baina ya
Rais Jakaya Kikwete na Mfalme wa Dubai Shekh Makthum na Jumuiya ya falme za kiarabu.
Alisema utekelezaji wa miradi hiyo ni ahadi ya Rais Kikwete
kwa maeneo ya wafugaji ambapo alisema azma yake ni kuona tatizo la maji katika
maeneo ya wafugaji linamazika na kuona mifugo na wafugaji wakinenepa.
Aliwataka wananchi wa Loliondo kuitunza miradi hiyo kwa
faida yao na mifugo yao huku wakitumia muda mwingi kwa kazi za maendeleo ya
loliondo.
No comments:
Post a Comment