Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini - TFF, Jamal Malinzi amewatakia kila
la kheri Wawakilishi pekee wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho
Barani Afrika (CC) timuYoung Africans katika mchezo wake wa marudiano
dhidi ya timu ya Etoile du Sahel utakaochezwa kesho nchini Tunisia.
Katika
salamu zake Malinzi amesema ,Young Africans wakiwa ndio timu wawakilishi
pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki katika michuano ya kimataifa
barani Afrika wanapaswa kupambana kuhakikisha wanasonga mbele katia
hatua inayofuata.
Katika
mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam,
Young Africans ilitoka sare ya bao 1- 1 na Etoile du Sahel, na mshindi
wa jumla kwa mchezo wa huo, atacheza hatua ya mtoano (Play-off) dhidi ya
timu zitakazokuwa zimetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa (CL) kuwania
kufuzu kwa hatua ya makundi.
Mchezo
huo wa marudiano utapigwa kesho jumamosi katika dimba la Olympique de
Sousse katika mji wa Sousse kuanzia majra ya saa 3 kamili usiku kwa saa
za Afrika Mashariki na Kati.
VPL KUENDELEA WIKIENDI HII
Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii
kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku michezo
mitatu ikichezwa siku ya jumamosi na michezo mingine mitatu ikichezwa
siu ya jumapili.
Jumamosi
katika Uwanja wa Sokoine wapinzani wa jiji la Mbeya, Prisons FC watakua
wenyeji wa wagonga nyundo Mbeya City mchezo utaochezwa majira ya saa 10
kamili kwa saa za Afrika mashariki na Kati.
Katika
Uwanja wa Nangwanda Sijaona wenyeji timu ya Ndanda SC watawakaribisha
wakata miwa wa Kagera Sugar, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa
wenyeji wa maafande wa JKT Ruvu mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa
Mkwakwani.
Jumapili
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaa, Simba SC watawakaribisha
Azam FC, mchezo ambao unatabiriwa kuwa na upinzani mkali kusaka nafasi
ya pili ili mwakani kuweza kuwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe
la Shirikisho barani Afrika.
Jijini
Tanga wagosi wa kaya Coastal Union watawakaribisha timu ya Stand United
kutoka mjini Shinyanga, mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani,
huku kwenye Uwanja wa Manungu mjini Morogoro wenyeji Mtibwa Sugar
wakiwakaribisha maafande wa Ruvu Shooting.
AMBROSE, NGASA WACHEZAJI BORA VPL MACHI, APRILI
Mchezaji
James Mwasote Ambrose wa timu ya Tanzania Prisons FC amechaguliwa kuwa
mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Machi 2015 kufuatia
kuwapiku wachezaji wengine waliokua wakiwania nafasi hiyo.
Jopo
la maalum la makocha ambao hutafuta wachezaji bora kwa kila mchezo na
kisha kujumlisha alama za mchezaji kwa kila mchezo na kumpata mchezji
bora wa mwezi, ndio hufanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila
mwezi.
Mshambuliaji
wa Young Africans Mrisho Ngasa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi
Kuu ya Vodacom mwezi Aprili kufuatia kuwapiku Amos Edward, Frank Domayo
na Emmanuel Okwi baada ya kupata alama nyingi za jumla za mchezaji bora
kwa kila mchezo.
Kwa
kuibuka wachezaji bora wa mwezi Machi na Aprili, James Ambrose na
Mrisho Ngasa watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kwa kila mmoja
kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodaom.
NB:
Kesho jumamosi tarehe 02 Mei 2015, kutakua na mkutano na waaandishi na
habari saa 5 kamili asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF - Karume,
waandishi wote wa habari mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment