Na
Antony Sollo Shinyanga
JESHI la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga linawashikilia watu
sita kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya
Albino wakiwa katika harakati za kuviuza viungo hivyo.
Akizungumza Ofisini kwake Mkuu wa kituo cha
Polisi wilayani Kahama Leonard Nyandahu, alisema kuwa watu hao walikamatwa May
21 mwaka huu majira ya saa 7 mchana katika nyumba ya kulala wageni ya MAJI
HOTEL, iliyopo katika maeneo ya Phantom kata ya Nyasubi wilayani Kahama.
Nyandahu amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Bahati Kirungu(56) mwalimu wa
shule ya msingi Katungulu kata ya Wendele, Wilayani Kahama ,Mhoja John(24)
mkulima mkazi wa Isagehe Nzega,Biliya Busanda(39) mkulima mkazi wa Mogwa Nzega.
Wengine ni Shija Makandi(60) mkulima mkazi wa Isagehe Nzega,Regina
Kashinje(40) mkulima mkazi wa Isagehe Nzega,na Aboubakary Ally(25) ambaye ndiye
aliyewahifadhi watu hao mkazi wa Isagehe Nzega.
Nyandahu amesema mnamo tarehe 19.5.2015 asubuhi mkuu wa upelelezi kituo cha
Polisi Nzega alipata taarifa za mtu kuwa anauza viungo vya Albino na mtego wa
kumkamata ulifanyika bila mafanikio badala yake akahamishia biashara hiyo
wilayani Kahama.
Aidha Nyandahu amesema maafisa upelezi mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na
Afsa upelelezi kituo cha polisi Kahama walifuatilia nyendo za watu hao na ndipo
mtego wa kuwakamata watu hao ulipowekwa na kuwanasa.
Hata hivyo Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga linaendelea
kuwashikilia watu hao kwa mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na kuubaini mtandao huo
ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria
No comments:
Post a Comment