Mkurugenzi wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja katika mradi wa Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika Ijumaa ya Mei 22, katika Hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo viongozi wa serikali. (Na Mpigapicha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida, taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services,
inayojihusisha na mikopo, imeanzisha huduma mpya ya kukopesha
viwanja watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni za kawaida na wajasiriamali
wa aina zote.
Kuanzishwa
kwa huduma hiyo mpya kumetokana na taasisi hiyo kupania kuboresha maisha ya
Watanzania, likiwamo kundi la wajasiriamali ambalo limeendelea kusahauliwa na
kampuni nyingi kupewa mikopo.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki katika uzinduzi huo uliofanyika katika Hoteli ya Serena,
Mkurugenzi wa Bayport Financial Services, John Mbaga, ni kusudio lao kutoa
fursa ya watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni na wajasiriamali wakipata
nafasi ya kutimiza
ndoto
za kumiliki ardhi nchini Tanzania.
“Huduma
yetu katika mradi wa Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani, fomu zake zinapatikana
katika matawi yote ya Tanzania Bara, huku fomu za kukopeshwa viwanja hivyo
zikipatikana kwa wiki mbili, kuanzia Mei 22 hadi Juni 10 mwaka huu.
“Si
lazima uwe mtumishi wa umma ili uwe na sifa ya kukopeshwa viwanja, ila hata
wajasiriamali nao wamekumbukwa katika huduma hii nzuri kwa Watanzania wote,
hivyo ni wakati wao sasa kuiunga mkono taasisi hii ili iweze kuwakomboa na
kuwakwamua pia,’ alisema Mbaga.
Akimwakilisha
Mkuu wa wilaya ya Kibaha katika uzinduzi huo, Afisa Mipango wa wilaya hiyo,
Obed Katonge, alisema kwamba Bayport imebuni huduma nzuri inayofaa kuungwa mkono
na Watanzania wote, hasa kwa kuingia kwenye sekta ya ardhi inayopanda thamani
siku hadi siku duniani kote.
“Serikali
hususan kwenye wilaya yetu ya Kibaha tumepokea huduma hii kwa mikono miwili,
ukizingatia kuwa wilaya yetu ni kati ya maeneo yanayokuwa kwa kasi, hivyo
tunaamini tutaendelea kushirikiana na Bayport kwa ajili ya kuwapatia mwangaza
wateja na wananchi wote kwa ujumla,” alisema Katonge.
Naye
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo,
alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya ni njia ya kunapanua wigo wao na
shabaha ya kuwafaidisha wateja wao na Watanzania wote kwa huduma na bidhaa
zilizothibitishwa kwa ubora zaidi.
“Bayport
ilikaa na kufanya tafiti kadhaa zenye nia ya kujenga jamii na kuinua uchumi wa
Watanzania wote, hivyo tukaona ipo haja ya kufungua ukurasa huu wa kukopesha
viwanja, huku wateja wetu wakitakiwa kulipa kila mwezi katika vipindi vya miezi
24,
ambapo kiwanja cha chini kabisa kinapatikana kwa Sh 1,700,000 na nzuri zaidi
wateja wetu wanaweza kuona huduma nyingine nzuri za mikopo
kwa kupitia tovuti yetu yawww.kopabayport.co.tz ,” alisema Cheyo.
Naye
Meneja Bidhaa wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema makato ya
kiwanja chenye thamani ya Sh 1,400,000 kwa mjasiriamali ni 105,181.55, wakati
mtumishi wa umma akilazimika kukatwa Sh 73,684.49, huku akiongeza kuwa mtu
anaweza kupata kiwanja
kwa malipo ya fedha taslimu.
“Naomba
Watanzania wajitokeze kwa wingi kukopeshwa viwanja hivi ili watimize ndoto zao
za ujenzi wa nyumba, maana Bayport imekuja kwa ajili ya kuboresha maisha ya
Watanzania wote, maana tangu sasa kila mtu anaweza kuwa baba au mama mwenye
nyumba,” alisema Cheyo.
Mbali
na huduma ya mkopo wa viwanja, Bayport pia inatoa mikopo mbalimbali ya bidhaa,
mikopo ya fedha taslimu, bima ya elimu kwa uwapendao, huku mikopo yote hiyo
ikiweza kupatikana kwa njia ya mtadao wa www.kopabayport.co.tz.
No comments:
Post a Comment