Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wananchi mkoani Singida baada
ya kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais kwenye Uwanja wa Namfua leo.
(Picha na Loveness Bernard)
Umati wa
watu ukimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu baada ya kutangaza
nia ya kugombea nafasi ya urais kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida leo. (Picha
na Loveness Bernard)
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto) akiwa na mkewe Faraja kabla ya kuzungumza
na wananchi mkoani Singida wakati wa kutangaza nia.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alitangaza nia ya kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais katika sherehe
zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida.
Nyalandu alisema endapo atafanikiwa kuwa Rais, amedhamiria
kuwekeza zaidi kwenye rasilimali watu, ikiwemo kuliwezesha kundi kubwa la
vijana ambalo katika siku za hivi karibuni linaitwa bomu linalosubiri kulipuka
wakati wowote.
“Vijana si bomu ila kikubwa zaidi ni lazima tuweke
mazingira bora ya kuwawezesha watumie fursa zilizopo kufanya shughuli za
kuwaingizia vipato, tusipofanya hivyo hatutaweza kupiga hatua,” alisema.
Nyalandu alisema pia hataisahau sekta ya kilimo, afya,
elimu na miundombinu kwakuwa maendeleo hayo ndiyo yatachochea ukuaji wa uchumi
wa taifa na mtu mmoja mmoja.
Alisema serikali atakayoiongoza akiingia madarakani
itaendeleza mazuri yote yaliyopatikana kutoka kwa utawala wa serikali ya awamu
ya nne.
Nyalandu pia alikemea tabia iliyoanza kujitokeza kwa baadhi
ya wanaosaka nafasi ya kuteuliwa na CCM kuwania urais kuwarushia vijembe wenzao,
kwamba havina faida kwa chama na taifa.
Alisema akiingia madarakani ataendeleza pale rais aliyepo
madarakani atakakoachia.
No comments:
Post a Comment