Na Bryceson Mathias,
Dodoma
MWANASIASA Machachari na
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni,Tundu Lissu, ameponda Safari ya
Matumaini ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM),
Edward Lowassa, akidai si ya Matumaini, ni ya Matumizi.
Lissu alisema hayo katika
Mkutano wa Hadhara alioufanya mkoani Dodoma jana katika Viwanja vya Barafu, ambapo pia
alidai Watawala hao hawana uwezo tena wa kutawala kama kwanza.
Akiainisha Ishara za Watawala
kushindwa kuongoza mbele ya Umati wa Wakazi wa Dodoma, Lissu alisema kuwa ni pamoja na
Migogoro na Migomo kila Kona, ambapo Wafanyabiashara, Madereva, Wanavyuo,
Walimu, Wakulima na Wauguzi na Madaktari, safari hii waliiasi Serikali ya CCM.
Lissu ambaye alikuwa
akihamasisha kujiandikisha katika Daftari la Kuduma la Kura, aliwakumbusha
Wananchi akisema, mmewasikia wasaka Urais wa CCM wanaotoka Chama kimoja wanavyotofautiana
kwa Kauli Mbiu, kila mmoja ana yake! Mkiona hayo, Ukombozi umefika.
“Lowassa amesema, ana Safari
ya Matumaini; Safari hiyo si safari ya Matumaini ila ni Safari ya Matumizi, …Naibu
Waziri wa Fedha, Mwigulu Mchemba, amesema, tutavushwa Ng’ambo, wengine acheni jamani…Watu
wanasema, ‘Ukimwamsha aliyelala Utalala Mwenyewe”.alisema Lissu na wananchi wakshaangilia
na kucheka.
Lissu alijinasifu akisema, Dhambi
kubwa kuliko zote ambayo Watawala wa nchi hii wamewafanyia Watanzania, ni
kuifanya nchi yetu kuwa Nchi ya watu Ombaomba, na ndiyo maana nimemsikia Mgombea
Urais wa CCM, Makongoro Nyerere, akijinadi ‘tusiwape nchi hii Vibaka’.
Alisema, “Rais Jakaya
Kikwete, anaomba, Mawaziri wake wanaomba, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi Wanaomba,
Wakuu wa Mikoa wanaomba, Wakuu wa Wilaya wanaomba, na Polisi nao wanaomba!!
Jambo hili ni aibu kwa Taifa.
Lissu alidai; Taifa hili limechafuka
sana kwa Uovu ukiwemo, Wizi, Rushwa, Ufisadi na Mauaji ya Kutisha yanayomwaga
Damu za Watanzania, hivyo linatakiwa kusafishwa… na njia pekee ni kujiandisha
kwenye daftari la kudumu la wapiga Kura, ili 25/10/2015, mtumie haki yenu.
Hata hivyo, Lissu
alijigamba kwamba, Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamejipanga vizuri
kuchukua Dola, na ndiyo maana walitoka nje wakipinga Katiba na inayopendekezwa
na kura ya maoni, kwamba isingewezekana Aprili 30, sasa nani Mkweli?.alihoji.
No comments:
Post a Comment