NA ELIZABETH JOHN
MKURUGENZI wa bendi ya
Yamoto, yenye maskani yake Temeke jijini Dar es Salaam, Said Fella ‘Mkubwa
Fella’ amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa Escape One
Mikocheni kuwaunga mkono wasanii wa bendi hiyo katika uzinduzi wa ngoma yao
mpya.
Uzindizi wa ngoma yao mpya ya
‘Cheza Kimadoido’ unatarajiwa kufanyika Jumamosi katika ukumbi huo huku
kiingilio kikiwa ni shilingi 10,000.
Kwa mujibu wa Mkubwa Fella,
wasanii ambao watasindikiza uzinduzi huo ni bendi ya Mapacha Watatu, Tunda Man,
Madee, Chege na Temba.
“Tunatakiwa kuwasapoti vijana
wetu ili muziki wetu uendelee kukua, pia tunashukuru kwa kuipokea ngoma hii kwa
mikono miwili tunaomba tuendelee kupeana sapoti kazika soko la muziki wetu,”
alisema.
Bendi hiyo ambayo inafanya
vizuri katika soko la muziki huo, inaundwa na wasanii wanne ambao ni Aslay,
Maromboso, Beka One na Enock Bella.
No comments:
Post a Comment