CHIPUKIZI wa muziki wa kizazi kipya nchini, kutoka Nyumba
ya Kukuza vipaji Tanzania (THT), Rubby amewapa nafasi wapenzi wa kazi yake
kuitathimini video ya wimbo wake wa ‘Na Yule’ ambao ameusambaza juzi katika
vituo mbalimbali vya televisheni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rubby alisema kuwa, kazi
hiyo anaamini itafanya vizuri kutokana na mazingira ambayo ametumia kuitengenezea.
“Nina amini nimefanya kazi nzuri, ila kwa sababu nina
mashabiki ambao wanafatilia muziki wangu nitaomba wanipe maono yao katika kazi
hii ili nijifunze na nisikirudie katika kazi nyingine,” alisema.
Alisema kuwa anaomba wapenzi zake waendelee kumpa sapoti
katika kazi zake ambazo zinakuja kwani kuna kazi nyingi ambazo anatarajia
kuzisambaza.
Rubby ametamba katika soko la muziki huo kutokana na
kusambaza ngoma yake ya ‘Na Yule’ ambayo imefanya vizuri sokoni kutokana na
ujumbe uliopo ndani yake.
No comments:
Post a Comment