Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dares Salaam leo kuhusu nia yake ya kutaka kuwafungulia mashtaka makada wa CCM kwa madai ya kuanza kampeni mapema.
Dar es Salaam, Tanzania.
MWENYEKITI wa Democratic
Party, (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, anatarajia kutinga mahamani kukifungulia
mashtaka Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na makada wake sita, akidai wameanza
kampeni za uchaguzi mkuu mapema.
Makada
hao ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, na Waziri mstaafu Frederick Sumaye,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe.
Wengine
ni William Ngeleja, Waziri wa Chakula na Kilimo Stephen Wasira na Naibu Waziri
wa Sayansi na Teknolojia January Makamba, ambao wote hao waliwahi kupewa adhabu
Februari 18 mwaka jana, kwa kosa la kuanza harakati za kuwania nafasi ya urais.
Akizungumza
na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mchungaji Mtikila, alisema
kuwa suala la makada hao sio la kuliacha hivi, hivi, kwani linagusa maslahi ya
nchi.
Alisema,
amefikia hatu hiyo baada ya kujiridhisha kuwa wanaushahidi wa kutosha juu ya
vitendo vya makada hao kwenda kinyume na sheria za uchaguzi.
Mchungaji
Mtikila, alisema makada hao wamejiingiza kwenye vitendo vya matumizi makubwa ya
fedha kwa kusafirisha watu kwenda maeneo mbalimbali huku watu hao wakilewa na
kulala bure.
“Wanasheria
wetu hivi sasa wanapinda migongo katika kukamilisha mchakato wa shauri hili n
kwamba litakapokamilika wakati wowote kuanzia sasa tutawaita kuwaeleza kwamba
linakwenda mahakamani.
“Baadhi
ya watu wanatafuta utawala kwa sababu ni meno ya kumung’unya rasilimali za nchi
hii,”alisema Mchungaji Mtikila.
Mchungaji
Mtikila alisema kuwa hatua hiyo ya kukifikisha chama hicho pamoja na makada
wake hazitaishia hapo bali watafanya hivyo hata katika vyama vingine pindi
watakapobaini vimeingia kwenye vitendo vya matumizi ya fedha chafu katika
upataji wa wagombea wake.
“Kumekuwa
na umwagwaji kubwa wa mabilioni ya fedha chafu kwa ajili ya kusaka madaraka
jambo ni sawa na uhalifu na uhani,”alisema Mchungaji Mtikila.
No comments:
Post a Comment