HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 08, 2015

TFF YAUPONGEZA UONGOZI WA COASTAL UNION


Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia ametuma salama za pongezi kwa uongozi mpya wa klabu ya Coastal Union uliochaguliwa mwishoni mwa wiki.

Katika salamu zake kwa Mwenyekiti mpya wa klabu hiyo Dr. Twaha, Karia amesema anawapa pongezi wa kuchaguliwa na kupewa heshima hiyo na wanachama wa Coastal Union katika kuitumikia klabu yao.

“Kikubwa wanachopaswa kufanya kwa sasa ni kuodokana na makundi ya aina yoyote, na kuifanya Coastal Union kuwa kitu kimoja na kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom” alisema Karia.

Aidha Karia amesema, TFF itashirkiana na uongozi mpya katika utendaji wa kazi na kuleta maendeleo katika mpira miguu nchini.

Klabu ya Coastal Union yenye makazi yake jijini Tanga ilifanya uchaguzi wake mwishoni mwa wiki na kuwapata viongozi wake wapya, akiwemo mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wa Kamati ya Utendaji.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment

Pages