HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 01, 2015

DOUBLE TREE HOTEL WATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTOT WETU TANZANIA


 Meneja Mkuu wa Double Tree hotel Ndugu Ian Mclachlan Akimkabidhi  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Msaada wa Magoro 80 .Akipokea Msaada huo Mkuu wa Wilaya Mh Makonda ameushukuru Uongozi wa Msaada huo.Kutoka Hotel ya Double Tree ya Jijini Dar es salaam.

Msaada huo umekabidhiwa na Mkuuwa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda.Kituo Hicho kinacholea Watoto na vijana wa Mitaani na wanaoishi katika Mazingira Magumu kina Jumla ya Watoto Pamoja na Vijana 120 Kilianzishwa Mnamo mwaka 1998  Kwa lengo la Kuwasaidia watoto waliokosa Malezi na Huduma Mbalimbali za Kijamii.Kituo Hicho kinapatikana Kimara Suka pamoja na Kijiji cha Mazizini msata wilayani Bagamaoyo kinakabiliwa na Changamoto Mbalimbali hivyo Uongozi wa Kituo Hicho kinawaomba Watu binafsi na Wafadhili Mbalimbali kujitokeza kuwasaidia.

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akimkabidhi  Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto wetu tanzania Ndugu Evans Tegete Msaada  uliotolewa na Uongozi wa Double Tree Hotel .
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Katika Picha na Meneja Mkuu wa Double Tree hotel Ndugu Ian Mclachlan  (kushoto) Pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Hotel ya Double tree Ndugu Florenso Kirambata

No comments:

Post a Comment

Pages