HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 04, 2015

COASTAL UNION WAOMBA RADHI KUFUATIA VURUGU ZA MASHABIKI


UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umewaomba radhi wadau wasoka pamoja na shirikisho la soka nchini (TFF) kwa vurugu zilizotokeakwenye mchezo wa baina yake na Mbeya City uliofanyika mwishoni mwawiki uwanja wa Mkwakwani.

Mchezo huo wa ligi kuu Vodacom ulimalizika kwa  vurugu hadi kikosi chakutuliza ghasia kilipoingilia kati na kutumia mabomu ya machozikuwatawanya mashabiki wa soka waliokuwepo katika uwanja wa Mkwakwani.

Vurugu hizo zilitokea kufuatia mwamuzi,Erick Enock kutoka Arushakuamuru ipigwe penati kuelekea lango la Coastala union katika dakikaza majeruhi na kuiwezesha Mbeya City kusawazisha bao hivyo hadimatokeo kuwa sare ya fungana bao 1-1.

Coastal Union iliomba radhi katika barua yake iliyoandikwa na kutiwasaini na Mwenyekiti wake,Dr Ahmed Twaha kwenda kwa Katibu mkuu wa TFFna nakala kwa Rais Jamal Malinzi,afisa mtendaji mkuu bodi ya ligi nakatibu wa Chama cha soka mkoa wa Tanga (TRFA).

Aidha baada ya kutokea tukio hilo,Mwenyekiti huyo alisema alilazimikakuitisha kikao cha dharura cha kamati ya utendaji kujadili nini chakufanya na hatua za kuchukua kwa wale watakaobainika kuhusika kwenye
vurugu hizo.

Katika kikao hicho alisema kamati ya utendaji imelaani vurugu hizo naimeaziamia kuwachukulia hatua waliohusika“Tunaomba radhi kwa TFF naTRFA kwa matukio hayo yaliyofanywa oktoba
31,tunachukua ahadi klabu ya Coastal Union kufidia gharama za
uharibifu utakaothibitika na kuwachukulia hatu waliohusika”ilieleza sehemu ya barua hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages