Na Matukiodaima Blog, Ludewa
WAKATI wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Ludewa mkoani Njombe kesho jumanne wanapiga kura za maoni ili kumpata mgombea wa ubunge atakayezipa pengo lililoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita na na mgombea ubunge marehemu Deo Filikunjombe ,wananchi wa jimbo hilo wameomba wajumbe wa CCM kurudisha jina la mdogo wa marehemu Bw Philip Filikunjombe ili akawatumikie bungeni.
Wakati mchungaji wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKT) usharika wa Ludewa mjini mchungaji Tafuteni Mwasonya akidai kuwa tayari Mungu amekwisha wapatia wananchi wa Ludewa mbunge hivyo wagonje taratibu za kidunia zifanyike.
Kwani alisema anaetoa uongozi ni Mungu na kikubwa kwa wananchi wa Ludewa wanapaswa kuomba kwa Mungu badala ya kusikiliza wanadamu na kuongeza kuwa wanaemtaka ni yule ambae anaijua Ludewa vizuri na mwenye kuwaletea maendeleo .
Wakizungumza na mtandao kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema kuwa imani na matumaini yao ni kuona wajumbe wa mkutano wa CCM wanamchagua Philip Filikunjombe kuendeleza mipango mbali mbali ya kimaendeleo iliyoachwa na marehemu Filikunjombe.
Kwani wamesema kuwa Philip ambae alikuwa ni msaidizi na mratibu wa mipango ya jimbo hilo wakati wa uhai wa kakake Filikunjombe wanaimani kuwa ataweza kuwatumikia vema kama ilivyokuwa kwa kaka yake hivyo ili kuweza kuwafuta machozi yao juu ya maendeleo ya jimbo hilo wanaomba jina la Philip kuweza kuchaguliwa .
John Haule mkazi wa Mavanga akiungumza kwa niaba ya wananchi wenzake alisema kuwa ni wagombea zaidi ya watano wamejitokeza ila kwa wote hao bado wao kama wananchi wa jimbo hilo ambae wanaona anaweza kuwatumikia ni Filikunjombe .
" Tunaomba sana kama ingekuwa ni wananchi tunaamua ni nani awe mbunge wetu basi tusingehitaji kupiga kura za maoni kwa kauli moja tungempa Philip Filikunjombe .....ila kwa kuwa ni taratibu ndani ya CCM na sehemu ya Demkrasia basi tunalazimika kuzama katika maombi kuona azma yetu inatimia kwa kumpata yule tulie mtegemea baada ya kifo cha kipenzi chetu Deo"
Jumla ya makada 10 wa CCM waliochukua na kurejesha fomu na wanataraji kuchujwa katika mchakato huo wa ndani ya CCM ili kumpata mmoja atakapambana na mgombea wa Chadema mbali ya Philip Filikunjombe wengione ni Edgar Lugome.Johnson Mgimba,Emmauel Mgaya, James Mgaya, Jackob Mpangala, Saimon Ngatunga, Evaristo Mtitu, , Deo Ngalawa na Zephania Chaula,
Kwa upande wake Bw Philip akielezea vipaumbele vyake iwapo atachaguliwa katika mchakato huo wa kura za maoni ndani ya chama na wananchi kumchagua kuwa mbunge wao kwanza ni kuendelea mipango yote iliyoachwa na marehemu ambayo mipango mingi anaitambua na kuwa suala la nidhamu na uwajibikaji katika kazi kwake litakuwa ni msingi wa kweli wa kuwaletea wana Ludewa maendeleo .
Alisema Ludewa mbali ya kumpoteza mbunge wao bado wanayonafasi ya kuamua na kumchagua ili kuendeleza yote mazuri kwa ajili ya maendeleo yao na kuona kasi ya maendeleo katika wilaya hiyo inaendelea kukua kwa kasi na kuwaomba wana CCM kumwamini kwani hata waangusha na kuwa anachoomba wana CCM kumkopesha kura zao za ndio ili ndani ya miaka mitano awe kuwalipa maendeleo .
ELIMU
wakili wa mahakama kuu, mtafiti shahada uzamivu, katika sharia (PHD) Chuo Kikuu huria cha Tanzania , Shahada ya uzamili katika sharia (LLM), Chuo kikuu cha Stratchclyde, Uingereza, Diploma ya juu ya Mafunzo ya sheria kwa vitendo, Chuo cha Mafunzo ya Uwakili Tanzania, Dar es Salaam 2012, Stashada ya sheria (LLB), 2007 Chcha Tumaini Iringa, Cheti cha Lugha ya Kifaransa. Chuo kikuu cha Blida, Algeria 2004, Cheti cha Uandishi wa Habari, Dar es Salaam School of Journalism 2003.
Elimu ya kidato cha sita, shule ya sekondari Mzumbe 2002, Elimu ya Sekondari, Njombe Sekondari 1999, Elimu ya Msingi, Shule ya msingi Ludewa mjini 1995.
UZOEFU WA KAZI
mwanasheria mwandamizi, Mamlaka ya ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) 2012 mpaka sasa, Mkufunzi wa sheriaKikuu Huria cha Tanzania, 2010-2012, Mkufunzi wa Sheria, Chuo kikuu cha Matakatifu Augustino 2010-2912, Mkufunzi wa Sheria Chuo kikuu Tumaini Iringa 2007-2010.
UJASILIAMALI NA BIASHARA BINAFSI
Mkurugenzi na mmiliki wa Kampuni ya uwakili wa Reliance Legal Consultants, Dar es Salaam, Mkurugeni mmiliki wa kampuni ya usafiri ya Matatu Logistics, Dar es Salaam na Mkurugenzi na mdau wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Dar es Salaam.
Deo Filikunjombe pamoja na watu wengine watatu alifariki kwa ajali ya Chopa katika hifadhi ya Selou akitokea jijini Dar es Salaam kuelekea jimboni Ludewa mnamo Octoba 15 mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment