Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Jamal Malinzi amempongeza
mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo
DR kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza
ndani.
Samatta ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wanaocheza
Afrika baada ya kwashinda Robert Kidiaba (Congo DR) alieshika nafasi ya
pili na Bounedjah Baghdad (Algeria) aliyeshika nafasi ya tatu.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Samatta amekua mchezaji wa kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki kushinda tuzo kubwa barani Afrika.
Pamoja na kushinda tuzo hiyo, Samatta pia amejumuishwa katika kikosi
bora cha wachezaji wa Afrika kwa mwaka 2015 sambamba na Robert Kidiaba
(Congo DR), Sergie Aurier (Ivory Coast), Aymen Abdenmor (Tunisia),
Mohamed Meftah (Algeria), Sadio Mane (Senegal), Yaya Toure (Ivory
Coast), Yacine Ibrahim (Algeria), Andrew Ayew (Ghana), Mbwana Samatta
(Tanzania), Pierre-Emercik Aubameyang (Gabon) na Baghdad Bounedjah
(Algeria).
Mshambuliaji Mbwana Samatta alieyambatana na Katibu Mkuu wa TFF,
Mwesigwa Selestine wanatarajia kuwasili nchini leo saa 8 usiku kwa
shirika la ndege la Ethiopia.
No comments:
Post a Comment