Baada ya kusimama kwa wiki mbili kupisha michuano ya Kombe la
Mapinduzi visiwani Zanzibar, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania mzunguko wa
kumi na nne (14) unatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo 8
kuchezwa katika viwanja mbalimbali, huku timu 16 zikichuana kusaka
pointi 3 muhimu.
Jumamosi uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, Maafande wa JKT Ruvu
watawakaribisha Maafande wa Mgambo Shooting, Toto Africans
watawakaribisha Tanzania Prisosns uwanja wa CCM Kirumba, huku Stand
United wakicheza dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Kamabarage mjini
Shinyanga.
Uwanja wa Tafa jijini Dar es salaam, Simba SC watawakaribisha wakata
miwa wa Mtibwa Sugar saa 10 jioni, Mbeya City watakua wenyeji wa Mwadui
FC uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Coastal Union dhidi ya Majimaji
uwanja wa Mkwakwani, huku mchezo kati ya Azam FC dhidi ya African Sports
ukianza saa 1 usiku.
Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa mchezo mmoja uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam, ambapo Young African watawakaribisha Ndanda FC kutoka
Mtwara.
No comments:
Post a Comment