HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

April 14, 2026

Wanahabari 'kidedea' Tuzo ya Mwl. Nyerere Uandishi bunifu 2026


Mshahiri nguli duniani Abdilatif Abdalla akizungumzia safari yake kwenye ushahiri na harakati za ukombozi wa nchi za Afrika Mashariki.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda akizungumza kabla ya kuanza kwa hafla ya ugawaji wa Tuzo.


Mshindi wa Tuzo ya Tamthilia bora, mwanahabari Hamis Kibari.




Mshindi wa Tuzo ya Hadithi za Watoto Amina Abdulrahman.


Na Mwandishi Wetu 


WAANDISHI wa habari Hamisi Kibari na Bishop Hiluka kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), wameshinda Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu.


Katika tuzo hizo, Kibari ameshinda  Tuzo ya Tamthilia bora inayoitwa Ufalme wa Mabadiliko huku Hiluka akishinda Tuzo ya Riwaya bora iitwayo Waraka kutoka gerezani.


Washindi wengine ni kwa upande wa Ushairi ni Abdallah Ngereza kutoka Tanga, Hadithi za watoto na Amina Abdulrahman kutoka Zanzibar.


Tuzo hizo zilitolewa jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa The Super Dome Masaki na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu kutoka ndani na nje ya Tanzania.


Katika Tuzo hizo zilizogawanyika kwenye nyanja za Riwaya, Ushahiri, Hadithi za Watoto na Tamthilia ambapo mshindi wa kwanza hadi watatu walipata cheti na fedha.


Akitangaza zawadi za washindi, Mwenyekiti wa Tuzo hizo Profesa Penina Mlama, alisema washindi wa kwanza kila nyanja watapata sh. Milioni 10; Cheti na Ngao.


"Washindi wa pili kila nyanja watapata sh. Milioni saba na Cheti huku washindi wa tatu watapata sh. Milioni tano na cheti," alisema Profesa Mlama na kusisitiza kwamba idadi ya kazi zilizopokelewa mwaka huu ni 260. 


Huu ni mwaka wa nne mfululizo tangu kuanza kufanyika kwa Tuzo hizi zinazosimamiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ambazo kilele chake huwa ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere.


Mgeni rasmi katika Tuzo hizi alikuwa Mshahiri nguli, Abdilatif Abdalla (104) raia wa Ujerumani mwenye asili ya Afrika Mashariki akiongozana na mwenyeji wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda, Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo na Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Aneth Komba.


No comments:

Post a Comment

Pages