HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 05, 2016

AZANIA BANK YAFUTURISHA


Waumini wa dini ya Kiislamu wakipata futari iliyoandaliwa na Benki ya Azania ya jijini Dar es Salaam. 

 Wadau wa Benki ya Azania wakipata futari. 
 Wadau wa Azania Bank wakipata futari.
 Wateja na wadau wa Benki ya Azania wakipata futari.
 Wateja wa Benki ya Azania wakipata futari.
 Waumini wa dini ya Kiislamu wakipata futari iliyoandaliwa na Benki ya Azania ya jijini Dar es Salaam. 
 Waumini wa dini ya Kiislamu wakipata futari iliyoandaliwa na Benki ya Azania ya jijini Dar es Salaam.
Sheikh Mohamed Idd akitoa mawaidha katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Geofrey Dimoso akizungumza na wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya kufuturisha iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 


NA MWANDISHI WETU

BENKI ya Azania juzi iliandaa futari kwa ajili ya wateja wake na wadau wa benki hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, hata hivyo aliwakilishwa na Sheikh Mahamoud Abdallah Waziri.

Sheikh Waziri aliiasa jamii kujikita kwenye fungamano la Amani akisema hilo linapatikana kwa watu kukutana pamoja.
Aliwasihi Watanzania kudumisha utamaduni wa kujumuika pamoja, kufurahika au kubadilisha mawazo ili kuendeleza amani ambayo ndiyo tunu ya Taifa letu.

Aliupongeza uongozi wa benki ya Azania kwa kufanya tukio hilo adhimu la kuwakutanisha wadau mbali mbali, hasa katika kumi la mwisho la Mwezi mtukufu wa Ramadhani, akawasihi waendelee na utamaduni huo.

Naye Sheikh Muhammed Idd 'Abu Idd', alisema Saumu ni mchango ambao una malengo kwa anayefunga kuendelea na kuwa mtu mwema hata baada ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

"Moja ya malengo au hekima ya Saumu ni kumfanya mtu aishi vema na jamii yake kwamba Mwezi huo umeletwa ili kuwabdili watu kutoka kwenye uasi kwenda kwenye wema," alisema.

Aliongeza kusema kuwa lengo lingine la saumu ni kutengeneza afya kwa wafungaji jambo ambalo hata matabibu wamekuwa wakilisisitiza.

Naye Mkurugenzi wa Benki ya Azania, aliwapongeza wateja na wadau wao kwa kukubali mwito wao na kuhudhiria tukio hilo ambako anaamini wamepata vitu vya ziada kutoka kwa Masheikh waliotoa nasaha.




Alisisitiza kuwa benki hiyo ambayo ni wazawa kwa asilimia 100 itaendelea kuwahudumia watanzania katika mahitaji yao wanayohitaji, akawatolea wito wadau na wateja wao, wakiona kuna sehemu haijafikiwa kihuduma watoe taarifa na wao watalifanyia kazi mara moja.

No comments:

Post a Comment

Pages