Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama
(Mb) akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mifumo ya Kompyta wa Mfuko wa Pensheni
wa LAPF Bw. Yohana Nyabili kuhusu upatikanaji wa taarifa za michango ya
wanachama kupitia tovuti ya Mfuko www.lapf.or.tz na
simu za viganjani kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama
(Mb) akionyeshwa taarifa yake ya michango ya Hiari LAPF kwenye maonyesho ya
biashara ya 40 ya kimataifa jijini DSM. Anayemhudumia ni Afisa Mafao ya Mfuko
wa Pensheni wa LAPF Bi. Irene Michael.
Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama
(Mb) akipata maelezo kuhusu shughuli za uwekezaji za Mfuko wa Pensheni wa LAPF
pamoja na mipango ya Mfuko kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17, anayetoa
maelezo ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko Bw. James Mlowe.
Baadhi ya wanachama wa Mfuko
wa Pensheni wa LAPF kutoka Jeshi la Polisi wakipata maelezo mbalimbali ya Mfuko
kutoka kwa Afisa wa Mfuko Bw. Yohana Nyabili kwenye maonyesho ya biashara ya
kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini DSM.
Wanachama na wadau
mbalimbali wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakipata maelezo mbalimbali kuhusu
manufaa na huduma za Mfuko ikiwemo utaratibu wa kujiunga na kuweka akiba kwa
hiari kwenye Mfuko. Anayetoa maelezo ni Afisa mafao wa Mfuko Bi. Judith
Lupondo.


No comments:
Post a Comment