Balozi wa Kili Challenge Mrisho Mpoto atoa wito kwa watanzania kuitikia wito wa kuchukua jukumu la kupambana na Ukimwi kuwa ni jukumu la kila Mtanzania.
Hayo aliyasema usiku wa Jumamosi katika hafla ya “Auction” iliyoandaliwa na Mgodi wa dhahabu wa Geita “GGM” ili kuchangisha fedha za kuisaidia serikali dhidi ya mapambano ya Ukimwi.
Kili challenge ni mfuko unaoratibiwa na Mgodi wa dhahabu wa Geita GGM ukishirikiana na tume ya kupambana na Ukimwi nchini - TACAIDS na wadau wengine kwa kupandisha watu katika Mlima Kilimanjaro.
Fedha zinazopatikana zinagawanywa kwa asasi mbalimbali Tanzania ambazo zinajishughulisha na Mapambano dhidi ya Ukimwi. Hadi sasa zaidi ya Asasi 30 zimenufaika na mfuko huu kana vile TACAIDS, Benjamin Mkapa na nyinginezo, ambapo zaidi ya watu 500 kutoka katika Mataifa mbalimbali duniani wamepanda mlima Kilimanjaro kwa kupitia mfuko huu.


No comments:
Post a Comment