HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 31, 2016

MABALOZI WA USALAMA BARABARANI ARUSHA WAMSHANGAZA KAMANDA MPINGA

Kamanda Mohamed Mpinga akipokea "Birthday Surprise Cake " kutoka kwa Mwenyekiti wa RSA-Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwake (Mpinga) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016. PICHA NA GADIOLA EMANUEL.
 Kamanda Mohamed Mpinga wakishiriki shampeni na Mabaozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Balozi Vero Ignatus akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016. 
 Kamanda Mohamed Mpinga akikata "Birthday Surprise Cake " huku akishuhudiwa na Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Kamanda Mohamed Mpinga akipata picha ya pamoja na Mabalozi  katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.


Na Vero Ignatus, RSA Arusha

 Mabalozi wa usalama wa barabarani (Road Safety Ambassadors - Arusha) wamesherehekea sikukuu ya kuzaliwa ya Kamanda Mohammed  Mpinga jijini Arusha. 

Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Milestone Park -Sakina, imeandaliwa na kamati ya (RSA -Arusha) chini ya mwenyekiti wa mkoa Bi. Stella.

Rutaguza na kuhudhuriwa na wajumbe wa (RSA - Arusha) 
"Kwakweli mmenistua jamani sikutegemea kama mmeniandalia jambo kubwa kama hili ,nilijua nakuja kukutana tu na mabalozi ili kufahamiana na kuongelea maswala yetu ya usalama barabarani "alisema Mpinga.  

DCP Mpinga mbaye yupo kikazi jijini Arusha alikutana na mabalozi wa usalama barabarani,kwa lengo la kuongelea na kujadili  maswala ya usalama barabarani na mabalozi hao,ambao kazi yao kubwa ni kuelimisha
jamii,kukemea na kuripoti matukio yanayoathiri usalama barabarani,na kushawishi mabadiliko ya tabia ,sheria na sera. 

Amezungumzia changamoto iliyopo kwa sasa kwa utoaji wa risiti pale dereva anapotakiwa kulipa faini kutokana na makosa yanayofanyika barabarani, amesema kuwa mfumo huo wa kieletroniki tayari umeshaanza kutumika jijini Dar-es-salaam na hivi karibuni mfumo huo utaanza kutumika katika mikoa sita iliyopewa kipaumbela kabla ya mwaka huu
kumalizika. 

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Arusha,P wani, Morogoro, Mbeya, Dodoma, na Mwanza, na amewataka askari wa usalama barabarani kutumia lugha njema kuwaelewesha madereva pale wanapohitaji kupewa risiti za (EFD) ili waweze kutambua changamoto hiyo kwa sasa ambayo serikali inalishughulikia.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Bushbuck safaris Bw. Mustafa Panju amemuomba mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Arusha SSP. Eng. Nuru Suleimani ampe ruhusa ya kutoa mafunzo kwa askari wa usalama barabarani
Arusha kuhusu huduma kwa mteja. 

"Nipo tayari kutoa ofa ya mafunzo kwa askari wetu wa kikosi cha usalama barabarani ukinipatia nafasi ,na hii itasidia sana " Alisema Panju. 

 Naye mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa wa Arusha Bi.  Stella Rutaguza amempongeza Kamanda Mpinga katika siku yake ya kuzaliwa na kumtakia maisha marefu, yenye afya tele. 

Bi. Stella ameongeza kuwa katika mkoa wa Arusha kutakuwa na oparasheni Abiria paza sauti itakayofanyika kwa miezi mitatu lengo kuu likiwa ni kumjengea uwezo na kumuhamasisha dereva na abiria kuchukua tahadhari
kuepuka ajali.

Amesema kampeni hii inalenga kumfanya abiria atambue haki na wajibu wake ,akiwa kwenye basi APAZE SAUTI pale panapotokea uendeshaji hatarishi barabarani,na pia kumfanya dereva abadili mtazamo wake na kujenga utamaduni wa usalama barabarani, hii inamfanya dereva na abiria kuwa sehemu ya suluhisho la ajali za barabarani.


No comments:

Post a Comment

Pages