HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 31, 2016

Mume adaiwa kumchinja mke kwa wivu wa kimamapenzi!

Na Bryceson Mathias, aliyekuwa Muheza.

MWANAUME aliyetambulika kwa jina la Sadiki Andrea (35), wa Kitongoji cha Ngarani B, Kijiji cha Kwakifua, usiku wa Alhamisi Agosti 27, kuamkia Ijumaa 28, anadaiwa kumchinja, Rahel Nelson Mwagike (28), kwa sababu ya Wivu wa Mapenzi na kukimbia.

Akithibitisha kutokea Mauaji hayo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ngarani B, Ajuaye Noya, alisema tukio hilo la kuskitisha ni la kwanza katika eneo lao, hivyo kumeibuka hofu kubwa kiasi hata watoto hatumwi sokoni au Mtoni kuchota maji.

Akizungumzia Kifo hicho, Shemeji wa Marehemu aliyemuoa dada yake, George Mgaya, alisema Marehemu na Mtuhumiwa walikuwa marafiki wa kujificha, urafiki wao ukawa wazi, wakaanza kuishi pamoja na baadaye wakaanza kuhitilafiana, mwanaume akimhisi vibaya anapohudumia wateja wake klabuni.

“Kwa hitilafu hizo za mara kwa mara zilimchosha Marehemu na kuamua waachene, lakini mwanaume inaonekana hakuafiki, akawa akifika kwa Mke na wakati mwingine akilala, tukijua ni nia kwa nia ya kurejesha upya uhusiano wao”.alisema Mgaya.

Mgaya anadai, Siku tukio asubuhi Mgemaji wa Pombe (Mnzazi), Yohana alimaarufu Kanumba, alifika nyumbani kwa marehemu kama ilivyo ada, kuchukua Dumu la kujaza ambalo huwekwa nje ya Nyumba ili kwenda kugema.

Aliporudi na Pombe ili wapimiane, kila alipopiga hodi hakujibiwa, akalazimika kuingia ndani ili amuamshe, na kumgusa miguu alishituka akakimbia kunfuata shemeji yake Mgaya hatua 10 kutoka nyumbani kwa marehemu, na alipomfunua kichwani, alikuwa amekufa akiwa amekatwa Mishipa miwili ya Kooni, Kisu akiwa amekilalia.

Majirani waliohojiwa akiwemo Mgaya wamedai, usiku huo walisikia sauti kubwa ya Muziki lakini hawakushituka kufikiria uwezekano wa kutukia tukio hilo kutokana na wao kuwa na tabia hiyo, kumbe siku hiyo ndiyo aliyokuwa anatimiza azma yake.

Kamanda wa Polisi wa Wilaya (OCD), Innocent Seksi, amethibitisha kutokea kwa Mauaji hayo, na kwamba licha ya mtuhumiwa kukimbia baada ya kufanya tukio hilo! Hatimaye amejisalimisha kituoni hapo na wamemtia mbaroni wakisubiri kumfikisha mahakani kwa tuhuma za mauaji.

Wakati huo huo wakati wakiwa kwenye Mazishi ya Marehemi katika Kijiji cha Ngarani A kwa mzazi wake marehemu, Kijana mmoja naye alianza kuleta fujo na kutoa vitisho vya kutatishia kuua, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ngarani B, Noya kwa mara nyingine akishirikiana na Viongozi wa Ngarani B walimchukua na kumpeleka Polisi ambako ametupwa Lupango.
 

No comments:

Post a Comment

Pages