Ofisa Usalama Viwanjani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), anayetambuliwa na FIFA, Inspekta Hashim Abdallah akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu namna jinsi Jeshi la Polisi lilivyojipanga kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa mechi ya Simba na Yanga Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Ndugu Watanzania Jumamosi, tarehe 25/02/2017 saa 10.00 jioni Uwanja wa Taifa tutakuwa na mchezo mkubwa wa kati ya Simba SC na Yanga FC.
Ikumbukwe kuwa mchezo uliopita wa timu hizi uliochezwa
kwenye uwanja huu tarehe 1/10/2016 zilitokea vurumai zilizosababisha Serikali
kuufungia Uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu. Vurugu hizo zilisababisha uharibifu
wa miundombinu ikiwemo uvunjifu wa viti, mageti na mbaya zaidi baadhi ya watu
walijerehuliwa.
Tunaomba waandishi na wadau wote tushirikiane kuelimisha
umma wa wapenda michezo kuwa Michezo ni Furaha, Amani na Upendo.
Kuelekea
mchezo ujao tungependa kueleza yafuatayo:-
Tunawaomba wadau wote tujenge utamaduni wa kununua tiketi
mapema kwani mpaka sasa tiketi zinapatikana kupitia SELCOM. Hii itaondoa
msongamano na lawama zisizo za lazima.
Tunafahamu kuwa kuna changamoto za matumizi ya mfumo wa
Ki- elektroniki lakini hatuna budi kuendelea kuelimishana na kujifunza kwani
huko ndiko Dunia ilipo,tutakua watu wa ajabu leo tukisema hatuwezi kutumia
mfumo huu kisa changamoto hizi ndogondogo zinazojitokeza.
Tujiepushe na vurugu za aina yoyote siku ya mchezo kwani
Serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayepelekea uvunjifu wa amani siku ya
mchezo.
Kutakua na ulinzi wa kutosha ndani na nje ya Uwanja hasa
ukichukulia kuwa kuna kamera zenye uwezo wa kumuona kila mtu anayeingia
Uwanjani na kila anachokifanya. Tutapiga picha na kuzirusha kwenye TV kubwa ya
Uwanja kwa wale wote watakaobainika kuashiria/kutenda vurugu sheria itachukua
mkondo wake.
Tunatoa rai kwa waamuzi
waliopewa dhamana ya kuchezesha mchezo huu,wajue kuwa wana dhamana kubwa hivyo
ni vyema wakafuata kanuni na sheria za mchezo husika ili kuepusha malalamiko.
Mwisho napenda niwatakie mchezo mwema kwa timu zote wajue
kuwa Watanzania wanategemea burudani nzuri kutoka kwao,na niwaombe mashabiki
wakumbuke kuwa wajibu wao mkuu ni kuzishangilia na kuzipa hamasa timu zao na si
vinginevyo.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi
Mtendaji
Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Boniface Wambura yeye kwa upande wake,
alisema kwamba mchezo huo utaanza saa 10.00 jioni na kwamba mwamuzi atatangazwa
wakati wowote kuelekea mchezo huo.
Alionya
mashabiki kutofanya vurugu kwa sababu masharti ya kuufungulia yanakwenda
sambamba na kuchunguzwa kama jamii ya wapenda soka kama imejirekebisha baada ya
kutokea vurugu Oktoba mosi, mwaka jana.
Mtoa
Huduma wa Mauzo ya Tiketi
Meneja
Mauzo wa Kampuni inayotoa Huduma ya Kuuza Tiketi za Elektroniki, Gallus Runyeta
alisema kwamba wanatarajiwa kutoa huduma ambayo haitakuwa na changamoto kama
ilivyotokea huko nyuma.
Ofisa Usalama wa TFF/FIFA
Ofisa
Usalama wa TFF/FIFA, Inspekta Hashim Abdallah, alisema kwamba Jeshi la polisi
limejipanga vema kudhibiti kila aina ya fujo zinazoweza kujitokeza kwani wana
askari kama 300.
..…………………………………………………………………………........................
IMETOLEWA NA
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment