NA
MWANDISHI MAALUM, KATAVI
BODI
ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiongozwa na Mwenyekiti
wa bodi, Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara, leo Septemba 28, 2017
imetembelea
Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa ajili ya kukagua utendaji kazi ambapo ilipata
fursa ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi Izumbe Msindai.
Bodi
imepongeza utendaji kazi katika Hifadhi ya Katavi hususani suala zima la
kupambana na ujangili na juhudi zinazofanywa katika kuongeza idadi ya watalii
hifadhini.
Aidha,
Jenerali Waitara aliutaka uongozi wa hifadhi kuongeza jitihada katika
kukabiliana na changamoto za mifugo ambayo ni kubwa kwa Katavi na pia
alipongeza uongozi wa mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali mstaafu Raphael
Muhuga kwa ushirikiano mkubwa anaotoa kwa hifadhi katika kupambana na mifugo
hifadhini.
Mapema
kabla, bodi iliweza kutembelea kituo cha mafunzo cha Mlele na kupokea taarifa
kutoka kwa Mkuu wa Kituo Mhifadhi Genes Shayo na kupata nafasi ya kuongea na
askari wapya wanaoendelea na mafunzo katika kituo hicho.
Jenerali
Waitara aliwataka askari hao kuwa na nidhamu, uwajibikaji, bidii na uzalendo
katika mafunzo yao na kuwa ni lazima waonyeshe kuiva ili waweze kupambana
vilivyo na changamoto ya ujangili katika Hifadhi za Taifa nchini.
Jenerali Waitara, akionyesha
kitu wakati yeye na wajumbe wa bodi walipotembelea enelo
wanakohifadhiwa Viboko
Jenerali Waitara akizungumza na
askari wanaopatiwa mafunzo kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi
Baadhi ya wajumbe wa bodi
waliofiatana na Jenerali Waitara
Baadhi ya askari wanaopatiwa
mafunzo ya ulinzi wa wanayamapori kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele
wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi za Taifa, (TANAPA),
Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (hayupo pichani),
alipowatembelea leo Septemba 28, 2017
Baadhi ya askari wanaopatiwa
mafunzo ya ulinzi wa
wanayamapori kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele wakimsikiliza Mwenyekiti
wa Bodi ya Hifadhi za Taifa, (TANAPA), Jenerali mstaafu George Marwa
Waitara (hayupo pichani), alipowatembelea leo Septemba 28, 2017
Jenerali Mstaafu George Waitara,
(kushoto) akipkewa na viongozi wa Hifadhi ya Taifa Katavi, alipowasili
mapema leo.
No comments:
Post a Comment