HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 07, 2017

Rostam wapagawisha Tigo Fiesta Morogoro

Msanii Richie Mavoko.
Wasanii Ben Pol na Jux wakishirikiana kuimba wimbo wao NAKUCHANA kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi.
Msanii Barnabas.
Msanii Country Boy.
Msanii Vanessa Mdee.
Msanii Nedy Music.
Msanii Nancy.
Msanii Mimi Mars akiimba kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro juzi.

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

WASANII wanaounda kundi la Rostan, ambao ni Roma Mkatoliki na Stamina, walipagawisha mashabiki wao katika tamasha la Tigo Fiesta, lililofanyika Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.

Wasanii hao walitoa burudani kwa staili ya tofauti na walivyozoeleka na kuwafanya mashabiki kulipuka kwa kelele.

Wasanii hao walipanda jukwaani kwa staili ya aina yake ambapo Roma alivaa jezi za timu ya Simba huku Stamina akiibuka jukwaani na jezi za Yanga. 

Wawili hao walionyesha umahiri mkubwa kwenye tamasha hilo kufuatia kuwatendea haki mashabiki lukuki waliojitokeza uwanjani kushuhudia tamasha la Tigo Fiesta. 

Wasanii wengine waliopagawisha katika tamasha la Tigo Fiesta ni pamoja na chipukizi ambao walionyesha uwezo mkubwa wa kutawala jukwaa.

Kwa upande wa wadhamini, Meneja wa Tigo kanda ya kati, John Tungaraza alisema anashukuru wakazi wa mji wa Morogoro kuitikia wito na kuonyesha ustaarabu kwa kuburudika kwa utulivu.

Pia aliendelea kusema "nawaomba wateja wa Tigo na wasiokuwa wa Tigo watembelee maduka yetu kote nchini waweze kupata bidhaa mbalimbali kwa punguzo ambalo lipo ndani ya msimu huu wa Tigo Fiesta" alimaliza kusema.

No comments:

Post a Comment

Pages