HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 06, 2018

BENKI YA CRDB YAKABIDHI MSAADA WA MADARASA MATATU NA MADAWATI KATIKA SHULE YA MSINGI MSASANI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Bi. Tully Mwambapa, akimuongoza mgeni rasmi Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta, katika hafla ya Benki ya CRDB kukabidhi msaada wa madarasa matatu pamoja na madawati 45 kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji maalumu katika Shule ya Msingi Msasani iliyopo jijini Dar es Salaam. 
 Muonekano wa jengo la kisasa lenye madarasa matatu yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum katika Shule ya Msingi Msasani.
Muonekano wa jengo la kisasa lenye madarasa matatu yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum katika Shule ya Msingi Msasani. 
 Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum wakisikiliza hotuba za viongozi wakati wa hafla hiyo.
Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum wakisikiliza hotuba za viongozi wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Msasani wakiwa katika hafla hiyo.
 Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum wakisikiliza hotuba za viongozi wakati wa hafla hiyo.
Kutoka kushoto ni Katibu wa Siasa, Uenezi Kata ya Msasani, Jane Mwambebule, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makangira, Suzana Msangi. 
Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum katika Shule ya Msingi Msasani wakiimba nyimbo wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta katika hafla ya kukabidhi madarasa matatu pamoja na viti 45.
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Msasani, Edward Mollel, akitoa hotuba yake.
Wanafunzi wakionyesha furaha yao baada ya kukabidhiwa jengo la madarasa matatu pamoja na viti 45.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Bi. Tully Mwambapa, akizungumza katika hafla ya Benki ya CRDB kukabidhi msaada wa madarasa matatu pamoja na madawati 45 kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji maalumu katika Shule ya Msingi Msasani iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meya wa Kinondoni Benjamini Sitta.
Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la madarasa matatu kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji maalum.
 Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum wakisikiliza hotuba ya Meya wa Kinondoni kupitia kwa mkalimali wao.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Bi. Tully Mwambapa, akimpongeza mgeni rasmi baada ya kutoka hotuba yake.
Mgeni rasmi akielekea katika uzinduzi wa jengo la madarasa matatu.
 Mgeni rasmi Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta (katikati), akikata utepe kuashiri uzinduzi wa jengo la madarasa matatu lililojengwa kwa msaada na Benki ya CRDB kwa ajili ya Wanafunzi wenye Uhitaji Maaulum katika Shule ya Msingi Msasani.
 Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta pamoja na Mkurugenzi wa Masoko Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, wakionyesha furaha yao sambamba na wanafunzi wa Shule ya Msingi Msasani baada ya kuzindua jengo la madarasa matatu.
 Bi. Tully Mwambapa, akimshukuru Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta, baada ya kuzindua rasmi jengo la madarasa matatu.
 Meya wa Kinondoni akipata maelezo kutoka kwa Bi. Tully Mwambapa.
 Bi. Tully Mwambapa (katikati), akionyesha furaha yake pamoja na wanafunzi wenye Uhitaji Maalum. Kulia ni Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Bi. Tully Mwambapa (kushoto), akimuonyesha Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta, moja ya ya chumba cha darasa lililojengwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wanafunzi wenye Uhitaji Maalum.
Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta (kulia), Mkurugenzi wa Masoko, Utafikti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Bi. Tully Mwambapa, Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Kinondoni, Bi. Shida Kiaramba wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum.
 Picha ya pamoja.
Mwalimu wa Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum akiwa darasani.
 Picha ya pamoja.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB, Bi. Tully Mwambapa, akikumbatiana na wanafunzi baada kupiga picha ya pamoja.
 Wanafunzi wakionyesha furaha yao.
Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB, Bi. Tully Mwambapa (kushoto), akiagana na Katibu wa Wazazi Kata ya Msasani, Maria Mtweve.
Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB, Bi. Tully Mwambapa (kushoto), akiagana na Katibu wa Siasa, Uenezi Kata ya Msasani, Jane Mwambebule. 

Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta, akiagana na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makangira, Suzana Msangi.

No comments:

Post a Comment

Pages