HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 04, 2018

CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TAWLA CHAKUTANA NA WADAU KUJADILI MABORESHO YA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI


Mkuu wa Usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Marison Mwakyoma akiongea na washiriki katika semeina ya kujadili sheria za usalama barabarani

Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA), Bi Isabella Nchimbi akiwasilisha hutuba ya ya mapendekezo ya mabadiliko ya sheria za usalama barabarani.


Picha ya pamja

................................................................................................

Kikosi cha Usalama barabarani kimesema sheria zilizopitwa na wakati zimetajwa kuwa chanzo cha ajari za barabarani nchini hivyo zinatakiwa zifanyiwe marekebisho.

Mkuu wa Usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Marison Mwakyoma alipokutana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA) ili kujadili mapendekezo ya mabadiliko na maboresho ya sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973. 
 
Amesema sheria ya usalama barabarani ilitungwa mwaka 1973na kufanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambayo ni ya muda mrefu ukilinganisha na mabadiliko yaliyopo ikiwemo magari kuongezeka pamoja na watu. 
 
Mwakyoma alisema sheria ya mwaka 1973 ikibadilishwa itaweza kupunguza ajali za barabarani alitolea mfano ukisoma sheria ya kufunga mkanda hakuna sheria haijamzungumzia abiria kama afunge mkanda na haimlazimishi imuadhibu kwa sheria gani. 
 
Pia kwa upande wa magari madogo sheria inasema anayetakiwa kufunga mkanda ni dereva na abiria aliyepanda mbele lakini aliyepanda nyuma haionyeshi kwenye sheria anatakiwa afunge mkanda Mwakyoma alisema abiria wanaopanda basi ambalo limejaa bado wanaengia kusimama hakuna sheria inaonyesha yule aliyesimama adhibiwe. 
 
Hivyo sheria hiyo ikirekebishwa na kuwekwa adhabu inayoendana na kosa husika watu wataogopa kuvunja sheria za usalama barabarani na itasaidia kupunguza ajari zinazoendelea kutokea. 
 
Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA), Isabella Nchimbi alisema utafiti waliofanya walibaini kuwa mapungufu katika sheria ya usalama barabarani vinavyosababisha ajali nyingi ikiwemo dereva kutumia simu ya mkononi wakati anaendesha gari akiwa barabarani. 
 
Mapungufu mengine uvaaji wa kofia ngumu kwa dereva na abiria wa pikipiki,uvaaji wa mikanda wakati ukiwa kwenye gari,kuendesha mwendo kasi na matumizi ya uvukaji kwenye vivuko .

No comments:

Post a Comment

Pages