HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 18, 2018

MANISPAA YA UBUNGO YASAINI MKATABA NA BENKI YA CRDB KATIKA KUTOA MIKOPO KWA VIJANA

Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mkataba na benki ya CRDB ambapo mikopo hiyo itatolewa kupitia benki hiyo.
Meya wa Ubungo, Bonjiface Jacob (katikati), akibadilishana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred (kushoto), jijini Dar es Salaam.


Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam, ndio Halmashauri pekee Tanzania nzima iliyotenga pesa nyingi kwa ajili ya mkopo kwa kinamama na vijana.

Hayo yamesemwa leo Jumatano 18/04/2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo  na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano na benki ya CRDB ambapo mikopo hiyo itatolewa kupitia benki hiyo.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imetenga kiasi cha 1.9+Bilioni, Boniface Jacob ametoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hii kwani idadi yao imeonekana kuwa ndogo ambayo ni, kwani mfuko huu ni nusu kwa vijana na nusu kwakinamama na 20% inakwenda kwa walemavu, Ubungo Manispaa itakuwa ya kwanza kwa utekelezaji wa agizo kwamba 20% tuwapelekee walemavu.

Kwa taarifa ya mratibu wa zoezi hilo, Wanawake waliojitokeza  ni 11,321, vijana idadi yake ikiwa ni 1124, kwa idadi hii ya vijana Mstahiki Meya ametoa wito kwa vijana kujitokeza zaidi na moja ya sifa ya kupata mkopo huu ni lazima mtu afungue akaunti Benki ya CRDB kwa maana hiyo CRDB wamejiongezea wateja, na Halmashauri imewahakikishia CRDB jambo hili ni zuri kwao.

Halmashauri ya Manispaa imetenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani ya mwaka mmoja nanusu waliyoitunza kwa uaminifu mkubwa ndio zikapatikana shilingi 1.9 Bilioni kwa ajili ya mikopo kwa kinamama na vijana.

"Nikiwa Manispaa ya Kinondoni tuliweza kutenga Milioni 800 kwa ajili ya mikopo kama hii, lakini Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ina muda wa mwaka mmoja na nusu tu lakini unaweza kuona kiasi tulichotenga kwa ajili ya mikopo kwa vijana na kinamama, ni kwa sababu tuko commited kuwasaidia wananchi wa Manispaa ya Kinondoni" amesema Meya Mhe Boniface Jacob.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk. Charles Kimei, Waheshimiwa Madiwani wa Ubungo na Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

No comments:

Post a Comment

Pages