NA SALUM
MKANDEMBA
BENKI ya Diamond Trust (DTB) na Kampuni ya Udalali
ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT Auction
Mart), zimeingia mkataba wa ushirikiano wa kikazi, unaoipa Suma JKT Auction Mart
mamlaka ya kukusanya madeni ya benki hiyo.
Hafla ya utilianaji saini ya makubaliano ya
ushinrikiano huo yalifanyika jana jijini Dar es Salaam, ambako Mkurugenzi
Mtendaji wa Suma JKT Auction Mart, Kapteni Farjara Mkojera, aliahidi utendaji
kazi makini, uliojaa weledi, nidhamu na uadilifu.
Kapteni Mjera alibainisha ya kwamba, Suma JKT Auction
Mart imejipanga katika kuzisaidia taasisi za kifedha kama DTB, kufanikisha
ukusanyaji wa madeni sugu kutoka wa wateja wao, ili kuibakisha na nguvu ya
kukabiliana na mchakato wa Tanzania ya Viwanda.
“Kuelekea Tanzania ya Uchumi wa Kati, taasisi za
kifedha zimekuwa wahanga wa kutorejeshwa kwa mikopo na kuzikosesha nguvu ya
kibiashara, kwa kuzingatia hilo, tukaja na Suma JKT Auction Mart, ambayo
imekuja kuziba mianya iliyoachwa na taasisi za udalali,” alisema. Mkojera.
Alifafanua kwamba, Kampuni nyingi za udalali zimekosa
weledi, nidhamu, uadilifu na utii katika ukusanyaji madeni, hali inayosababisha
wadaiwa wengi kutotendewa haki na kwamba kampuni yake imejikita katika
utekelezaji wa majukumu yak echini ya misingi hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Fedha DTB, Joseph
Mabusi, alisema makubaliano yao hayo (ambayo hayakuelezwa yatakuwa ya muda
gani), hayana maana kuwa benki yake ina madeni mengi yasiyolipika, bali
imevutiwa na dira ya Suma JKT Auction Mart.
“Ni makubaliano yanayoifanya Suma JKT kuwa sehemu ya
DTB, ikihusika moja kwa moja na ukusanyaji madeni, ingawa hayana maana kwamba
tuna wadaiwa sugu wengi. Taarifa za kifedha mwaka uliopita, ziliitaja DTB kama
moja ya taasisi chache zenye madeni machache yasiyolipika,” alisema Mabusi.
No comments:
Post a Comment