Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel akizungumza na waandishi wa Habari katika uzinduzi wa huduma
mpya itakayo wawezesha wateja wa mtandao wa Halotel kuangalia mechi za
kombe la dunia kupitia simu zao za kiganjani kwa gharama nafuu . Kulia ni Meneja Masoko wa Startimes David Malisa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa kwa pamoja wakionesha namna ambavyo mteja wa Halotel anavyoweza kuangalia mpira kwenye simu yake ya mkononi kupitia App ya Star times.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa pamoja katika uzinduzi wa Halotel na Startimes kuonyesha ishara ya ushirikiano.
-Bando hii itawawezesha wateja wa Halotel na StarTimes kutazama Soka kwenye simu zao kwa gharama nafuu sana.
Dar es Salaam, 28 Juni, 2018
Huku mshike mshike wa kombe la dunia ukiendelea kukolea, Kampuni
ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel kwa kushirikiana na Kampuni ya
StarTimes wameleta wamezindua huduma mpya itakayo wawezesha wateja wa
mtandao huo kuangalia mechi za kombe la dunia kupitia simu zao za
kiganjani kwa gharama nafuu.
Huduma
hii itawawezesha wateja wa Halotel na StarTimes kutazama Soka kwenye
simu zao kwa gharama nafuu sana, huduma hiyo inawapatia wateja intaneti
ya uhakika tena yenye kasi kwa masaa 24 bila kikomo.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda amesema huduma
hiyo itawawezesha wateja wa Halotel nchini nzima kufurahia kutazama
mechi za kombe la dunia kupitia simu za mikononi (Smartphone) kwa
urahisi na kwa gharama nafuu kwa kutumia intaneti ya uhakika tena yenye
kasi kwa masaa 24 bila kikomo.
“Kuanzia
sasa wateja wa Halotel wanaweza kupakua Application ya Startimes
kupitia simu zao za Android na watalipia kuanzia shilingi 2000 na
watapata GB 1 ambayo wanaweza kuitumia kuangalia mechi zote za kombe la
dunia kwa intaneti yenye kasi. Alisema Semwenda.
“Jinsi
ya kufanya malipo mteja wa Halotel anapaswa kufungua Application ya
Star times na baada ya hapo atafuata maelekezo ya kununua vifurushi
kuanzia vya siku, wiki hadi mwezi mzima,” Alihitimisha Semwenda.
Kwa
upande wake Meneja Masoko wa StarTimes Ndg. David Malisa
Alisema, “Ukiwa unatumia intaneti ya Halotel ni rahisi zaidi kulipia na
kutumia StarTimes App ambayo ina burudani na mechi zote za Kombe la
Dunia.
Kwa watumiaji wa mitandao mingine wanalipia maudhui pembeni na
intaneti au data pembeni, ukilipia huduma hii unakuwa umelipia maudhui
na intaneti kwa pamoja. Pia unaweza kutumia Intaneti hii bila kikomo kwa
masaa 24 hata bando inapoisha utaendelea kupata Intaneti ya kutumia
kwenye StarTimes App”. Alisema Malisa.
Hii
ni huduma ya kwanza kabisa Tanzania ambayo itamruhusu mteja kuendelea
kupata intanenti hata baada ya bando lake kuwa limekwisha. Ushirikiano
baina ya StarTimes na Halotel ni katika hatua ya kusogeza Burudani ya
kandanda la kimataifa katika Simu za Mkononi.
Kuhusu Halotel;
Halotel
ni chapa ya Viettel Tanzania Ltd, mwanachama wa Viettel Group. Viettel
ni kampuni kubwa ya mawasiliano ya simu nchini Vietnam yenye mapato
karibu dola bilioni 11 katika mwaka 2015. Mbali na Vietnam, Viettel
imewekeza katika sekta ya mawasiliano katika nchi 10 kote 03 mabara,
ikiwa ni pamoja na; Cambodia, Laos, Timor Leste, Myanmar kwa Asia
Msumbiji, Cameroon, Burundi, Tanzania kwa Afrika na Haiti, Peru ajili ya
Amerika. Halotel ilianza rasmi kutoa huduma Oktoba 15, 2015, na huduma
za simu katika maduka 30 kote nchini. Halotel nchini Tanzania tayari imepanua huduma za simu kwa mikoa yote vijijini na mijini.
Kuhusu StarTimes
StarTimes
ni kampuni ya Matangazo ya kidigitali inayoongoza Africa, ikihudumia
zaidi ya wateja milioni 10 katika bara zima. StarTimes inamiliki jukwaa
la maudhui lenye chaneli 480 zikiwemo chaneli za Habari, filamu,
tamthiliya, michezo, burudani, vipindi vya watoto, mitindo, dini na
vingine vingi. Matazamio ya Kampuni ni “Kuhakikisha kila familia ya
kiafrika inapata, inamudu, inatazama na kushiriki kwenye Uzuri wa
Televisheni ya kidigitali”
No comments:
Post a Comment