HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

October 22, 2018

ELIMU SAHIHI HAIJATOLEWA JUU YA MIFUKO NA TAASISI ZA KIFEDHA

NA KENNETH NGELESI, MBEYA
UKOSEFU wa elimu na Taarifa sahihi juu ya Mifuko na Mipango (Programu)ya ewezeshaji na Taasisi na vikundi vya kifedha vya kijamii nchini ni moja ya sababu zinizochangia kuwepo na maudhurio hafifu ya wananchi katika Moanesho ya taasisi hizo yanayoendelea  katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.
Hayo yamebainishwa na Mwakilishi ya Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF,Dismas Yusuph wakati wa  Majumuhisho ya Maonesho hayo huku akieleza kuwa elimu bado haijatolewa na wananchi hawana taarifa sahihi juu ya mifuko hivyo kuna haja ya watumishi kutoka taasisi zote zinazo jihusisha na masuala ya Mikopo na Programu kuwatembelea wananchi na kutoa elimu juu ya Mifuko hiyo.
Dismas alisema kuwa elimu sahihi haijatolewa ili kubaini fursa ili watu waelewe njia ya kupata mikopo kupitia mifuko inayo toa kwa jili ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.
‘Watu bado wanamitazamo tofauti kuhusiana na maonesha wengi wanadhani ni kwa ajili ya kuja kula nyama au kunywa hivyo kuna kazi kubwa lakini.. Mifuko inayotoa mikopo haijawajibika ipasavyo na ndiyo maana wananchi hawaelewi’ alisema Dismas.
Alisema kuwa Mifuko hiyo inawajibu wa kutoka ofisini na kuwafuata wananchi waliko ili kwenda kutoa mawazo na kuibua fursa za kiuchumi badala ya kuwasubili kufutwa ofisini.
Aidha katika hatua nyingine Yusuph aliwataka wazalishaji na wasindikaji wa bidhaa mbalimbali kutumia majina ya bidhaa kwa lugha ya Kiswali,badala ya Kiingeleza kama ambavyo wengi wao wanatumia kwani kufanya hivyo wanajitenga na soko.
‘Elimu inahitajika sana mfano watu wanatumia lugha ya Kiingeleza kuita majina ya bidhaa wanazo zalisha kufanya hivyo ni kujitenga na soko hivyo niwasii wasindikaji watumie lugha Kiswahili kwenye bidhaa zinazozalisha’ alisema Dismas.
Naye Nkurugenzi wa Taasisi ya (PASS) Nicomed Bohay alisema alisema suluhisho soko ya mazao ya kilimo lipo mikono mwa wakulima wenyewe kwa kubuni aina ya aina gani ya bidhaa wanaweza kuzalisha kutoka na mazao wanayo zalisha.
‘Mwarobaini wa soko la mazao ya wakulima ni wakulima wenyewe kwa kubuni bidhaa watakazo zalisha kutumia mazao wanayo zalishwa kwa mfano Mahindi unaweza kuzalisha chakula cha mifugo’ alisema Nicomed

No comments:

Post a Comment

Pages