Kundi la Rostam linalowashirikisha wasanii wawili Roma na Stamina jana
walipanda jukwaani kuimba pamoja na msanii Maua Sama wimbo unaotamba kwa
sasa ujulikanao kama IOKOTE kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama
Lote lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Tukio
hilo liliwafanya mashabiki walipuke kwa shangwe kwa namna wasanii wote
watatu walivyokuwa wakiiimba kwa pamoja na kufanya kionjo cha aina yake
na kwa ubunifu mkubwa.
Hii ilitokea kabla Maua
hajashuka jukwaani ndipo Rostam walipovamia jukwaa na kuimba wote, Na
mara baada ya kuimba wimbo huo, wakamalizia kuimba wimbo mwingine
walioshirikishana uitwao Kibamia.
Tamasha hili likiwa limemaliza mkoa wa sita usiku wa kuamkia jana, baada ya kupita mikoa ya Morogoro,Rukwa,Iringa,Songea,Mtwara na Kilimanjaro.
Wasanii
mbalimbali walinogesha tamasha hilo wakiwemo Weusi, Chege, Nandi, Me.
Blue,Chin Beez, WhoZu, Rosa Ree, Mavoko na wengine.
Kwa
upande wa shindano la kutafuta wasanii wenye vipaji Tigo Fiesta Supa
Nyota, msanii anayechipukia, Samson Msweta maarufu kama Samson Classic
aliibuka kidedea na atauwakilisha mkoa Kilimanjaro kwenye fainali za
Tigo Fiesta Supa Nyota mwaka huu jijini Dar es salaam.
Nao Wadhamini wa Tamasha hilo Kampun ya Tigo, Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka alisema ‘Mbali
na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya
thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#.
Promosheni ya Data Kama Loteitahakikisha
kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa
Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao
wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Bagaka alisema.
Wateja
wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila
wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa
kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz
Tamasha hilo litaendelea jumapili hii kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment