Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt
(Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi
funguo ya gari kwa wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Bi.Zeyana Rashid (kushoto) na Bi.
Fatma Mohammed Hassan (kulia) jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Wajane wa aliyekuwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi
Jumbe, Bi. Fatma Mohammed Hassan akiwasha gari baada ya kukabidhiwa funguo ya
gari hilo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst)
George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) nyumbani kwa wajane hao jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt
(Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiwa
katika picha ya pamoja na wajane wa
aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji
Aboud Mwinyi Jumbe, Bi.Zeyana Rashid (kulia) na Bi. Fatma Mohammed Hassan
(kushoto) mara baada ya kuwakabidhi gari la kuwahudumia.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt
(Mst) George H. Mkuchika (Mb)
akizungumza na familia ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Hayati Mzee Alhaji Aboud Mwinyi alipoitembelea familia hiyo jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Bi.Jane Kajiru (katikati) akizungumza na familia ya aliyekuwa Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mzee Alhaji Aboud Mwinyi jijini
Dar es Salaam.
Dar es Salaam, Tanzania
Serikali imewapatia
huduma ya usafiri wa gari wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe ikiwa ni sehemu ya
kutekeleza Sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Viongozi wa Kisiasa Na. 3
ya mwaka 1999 na Marekebisho yake ya mwaka 2005 inayoelekeza utoaji wa stahili
kwa wajane wa viongozi wa Kitaifa Wastaafu.
Akikabidhi gari
hilo kwa wajane hao jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) amesema
licha ya kuwa ni utekelezaji wa sheria lakini pia ni sehemu ya kuuenzi mchango
wa wastaafu katika ujenzi wa taifa letu.
Mhe. Mkuchika
amefafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria hiyo, stahili za wajane kwa viongozi wa
Kitaifa Wastaafu ni pamoja na malipo ya pensheni, malipo ya posho ya matunzo ya
kila mwezi, gharama za matibabu katika hospitali zilizomo nchini na kupatiwa
huduma ya usafiri.
Akizungumzia
mchango wa Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Mhe. Mkuchika amesema, alikuwa ni
kiongozi mahiri, jasiri na mchapakazi aliyeweza kutuliza machafuko yaliyowahi
kutokea Zanzibar na amefanya kazi ya kuwaunganisha watanzania.
Kwa upande wake,
mmoja wa mke wa Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Bi. Zeyana Rashid ameishukuru
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuihudumia familia
hiyo kwa kuipatia mahitaji yote muhimu.
Ziara za Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H.
Mkuchika (Mb) ni mwendelezo wa kuwajulia hali viongozi wa Kitaifa Wastaafu kwa
lengo la kuboresha huduma wanazopatiwa na Serikali.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 24 OKTOBA,
2018





No comments:
Post a Comment