HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

October 24, 2018

Wengi Wafurika Banda La Benki ya CRDB Kupata Maelezo Kuhusu Huduma za Kibenki kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Wajasiriamali-Simiyu

Maonyesho ya Ujasiriamali Kitaifa chini ya Uratibu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanafanyika Bariadi mkoani Simiyu katika viwanja vya Nyakabindi.


Maonyesho hayo yalifunguliwa rasmi na Mh.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Oktoba 23.10.2018 na kilele chake itakuwa Oktoba 28.10.2018, maonyesho hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya Ujasiriamali ikiwemo Benki ya CRDB.


Aidha kupitia Maonyesho hayo Wajasiriamali wamepata fursa nyingine tena ya kupata maelezo na ufafanuzi wa kina wa namna ambavyo Benki ya CRDB inasaidia sekta ya ujasiriamali kwa kuwapatia mikopo mbalimbali na kwa kuzingati kwamba Benki ya CRDB inao mtandao mpana wa matawi, ATMs na Wakala 'Fahari Huduma Wakala' mtandao umeenea nchini kote, mikoa yote, wilaya zote.


Pia Benki ya CRDB inatumia teknolojia ya kisasa ambapo pia wateja wake kama wajasiriamali wanaweza kupata huduma za kibenki za CRDB BANK kwa kupitia simu zao za mikononi, kwa Internet Banking, kwa TemboCards-visa, Mastercard na China Union Pay hata wakienda nje ya nchi.
Wananchi na wateja wakipata huduma za kifedha katika Banda la Benki ya CRDB wakati wa Maonyesho ya Kitaifa ya Wajasiriamali yanayoendelea mkoani Simiyu kwenye, viwanja vya Nyakabindi, Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, akifafanua jambo kwa maofisa wa benki ya CRDB alipotembelea banda lao.
Ofisa wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela, akimuunganisha, David Amon Haule, kwenye Huduma ya 'SimBanking Mob App' Mjasiriamali toka Kampuni ya Kusindika Kahawa "Mbinga Coffee Curing" kwenye Maonyesho ya Ujasiriamali Kitaifa yanayoendelea Mkoani Simiyu.

Wateja wakipata huduma kwenye banda la Benki ya CRDB.

Mkuu wa Mkoa Wa Simiyu, Anthony Mtaka, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB anayeshughulikia mikopo kwa wajasiriamali, Rachel Senni, namna Benki ya CRDB inavyosaidia maendeleo ya wajasiriamali nchini, mkuu wa mkoa huyo alitembelea Banda la Benki hiyo kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Wajasiriamali yanayoendelea mkoani Simiyu kwenye, viwanja vya Nyakabindi, Bariadi.
Cheti cha shukrani.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kulia), akisalimiana na Ofisa Uhusiano wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela, alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya wajasiriamali yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi-Bariadi mkoani Simiyu.

No comments:

Post a Comment

Pages