HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

October 25, 2018

NVRF wazidi kuifikia jamii Dar es Salaam



NA JOHN MARWA

TAASISI ya Network for Vulnerable Rescue Foundation (NVRF Sports Academy), wakishirikiana na Right to Play, wamezikosha nyoyo za wakazi wa mtaa wa Kigogo jijini Dar es Salaam kwa tamasha la uhamasishaji wa haki za watoto, vijana na wanawake katika jamii.

Tamasha hilo lilifanyika juzi kwenye viwanja vya Musako mtaa wa Kigogo Kati, ambako michezo mbalimbali ilifanyika.
Miongoni mwa michezo iliyofanyika ni Soka, Maigizo yenye kufundisha stadi za maisha na kutoa fursa ya kuwalinda watoto wa kike na vitendo viovu, na elimu ya jinsia kwa vijana.

Akizungumzia tamasha hilo, Meneja Mipango wa Right to Play Tanzania ambao ni washirika wa NVRF, Maria Mongi, alisema jamii isikate tamaa katika harakati za kuwakomboa watoto, vijana na wanawake kwenye changamoto zinazowakabili kila uchao.

“Pia kama Right to Play, tunafurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na NVRF katika kukwamua vikwazo mbalimbali vinavyoikumba jamii kwa kutoa elimu ya kujitambua na kijinsia kwa vijana na wanawake, huku wakiongeza hamasa ya haki ya mtoto kupata elimu,” alisema.

Mongi, alisema wanajivunia kuona ufadhili wanaoutoa kwa NVRF unatumika vizuri licha ya kuwa hautoshelezi, lakini wanaonyesha nia ya dhati ya kuisaidia jamii. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NVRF Sports Academy, Peter Mwangi, alisema amefurahishwa na uwepo wa washirika wao, kwani unawaongezea hamasa ya kuendeleza harakati za ukombozi kwa mtoto, kijana na mwanamke kupitia michezo.

No comments:

Post a Comment

Pages