Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiangalia mkungu wa ndizi unaolimwana wajasirimali kutoka Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) na Shirika la Floresta wakati wa ziara yake kukagua shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW).
Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile
akizungumza na wajasirimali kutoka Umoja
wa Vicoba Marangu (UVIMA) na Shirika la Floresta wakati wa ziara yake
kukagua shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo mkoani Kilimanjaro.
Na Mwandishi Wetu, Marangu Moshi
Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) wamemueleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile kuwa ndani mwaka mzima hawajawahi kumwona Afisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wala Wilaya kuja kuwatembelea katika vikundi vyao.
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo katika Shirika la Froresta linalojihusisha na utunzaji wa mazingira na Umoja wa Vicoba Marangu katika kujionea shughuli za uwezeshaji wananchi hasa wanawake kiuchumi.
Naibu Waziri Ndugulile amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Moshi Vijijini kuhakikisha wanawatembelea wajasiriamali na kuweka wazi vigezo vya uanzishaji vikundi na utoaji wa mikopo katika vikundi hivyo.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa ili kuwezesha kiuchumi hasa wanawake mamlaka husika zinatakiwa kutimiza wajibu katika kulifanikisha hilo.
Aidha Dkt. Ndugulile ameziagiza Mamlaka za SIDO, TFDA, na TBS kutoa elimu kwa wajasiriamali ili kuwawezesha katika kupata elimu juu ya uanzishaji wa biashara na kutengeneza wa bidhaa bora.
"Natoa agizo kwa kila ziara yangu wawepo SIDO, TFDA, na TBS waongozane na mimi ili kutatua changamoto na kero za wananchi kwa kila napoenda" alisisitiza Dkt. Ndugulile

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Floresta Mchungaji Winford
Mosha amemshukuru Naibu Waziri kuwatembelea na kuahidi kuendelea kushirikiana
na Serikali katika kutekeleza majukumu ya kuwawezesha kiuchumi wananchi hasa
wanawake.
Ameongeza kuwa uazishwaji wa vikundi na umoja wa
Vicoba umewasaidia wanawake wengi kujipatia kipato kinachowawezesha kutekelza
majukumu yao katika familiana jamii.
Naye mmoja wa wajasiriliamali Bi. Mary Mtei amesema kuwa wanamekuwa akikutana na changamoto mbalimbali katika kufikia malengo ikiweo unyanyasaji kwa wanawake ikiwa ni moja ya Ukatili wa Kijinsia unaowakandamiza wanawake.
Naibu Waziri Ndugulile yupo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tatu kufuatilia shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.

No comments:
Post a Comment