Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi,RAymond Mboya akiwa aameongozana na Madiwani wa Halmashauri hiyo kukagua shughuli za ukarabati unaoendelea katika kituo cha Afya cha Pasua mjini Moshi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya akijaribu kuzungusha moja ya vitanda vilivyowekwa katika wodi ya wazazi katika kituo hicho.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akizungumza mara baada ya kutembelea kituo cha Afya cha Pasua kujionea shughuli za ukarabati wa kituo hicho zinavyoendelea.
Baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wakiwa katika kituo hicho kuunga mkono shughuli za maendeleo .
Diwani wa kata ya Bomambuzi ,Juma Raibu kilipo kituo hicho cha Afya akizungumza mara baada ya ukaguzi .
Na Dixon Busagaga,wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
limeeleza kufanyia kazi tuhuma za ukiukwaji wa taratibu katika mradi wa
ukarabati wa Kituo cha Afya cha Pasua unaotajwa kupelekea upotevu wa fedha.
Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Moshi,Raymond Mboya wakati wa ziara ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya
Moshi walipotembelea kituo cha Afya cha Pasua kujionea ukarabati unavyoendelea.
“Kuna matatizo na hayo matatizo nimesema nije kwanza
kuangalia ,kwa kuwa bado hili swala liko kwenye vikao vya ndani tutatoa taarifa
yakikamilika kwenye vikao kwanza, ni
kwamba kuna taratibu hazijakaa vizuri kwenye mchakato mzima wa ukarabati wa
kituo cha afya.”alisema Mstahiki Mboya .
Alisema fedha zilizotumika katika ukarabati wa kituo hicho ni
fedha za serikali zinazotokana na kodi inayokusanywa kutoka kwa wananchi na
kwamba zinapotumika ni lazima baraza la Madiwani kufuatilia na kujiridhisha
kama zimetumika kwa utaratibu uliokusudiwa.
“Hizi fedha ni kodi zetu ,ambazo wakati mwingine zinaitwa
fedha za serikali sasa zinapotumika hapa ni lazima tuhakikishe zinatumika kwa
utaratibu uliokusudiwa na kwa utaratbu ambao hauta leta mashaka wala tatizo kwa
hiyo tusubiri mchakato na taratibu za vikao zitakapo kamilika tutawajulisheni”alisema
Mboya
Akizungumzia kuhusu ukarabati wa Kituo hicho ,Mstahiki Mboya
alisema hakuna mradi unaofanyika mahala popote
bila ya kupitishwa katika vikao halali vya baraza la Madiwani na kwamba
hadi kuanza kwa ukarabati kwa kituo hicho taratibu zilifuatwa.
“Tangu mwaka 2013 tulikuwa tunatenga fedha kwenye Bajeti ya
ujenzi wa vituo vya Afya kikiwemo kituo cha Afya cha Pasua ,na ilikua ni sehemu
ya upasuaji ,wodi ya kujifungulia kina mama,chumba cha mionzi ya X-ray na
chumba cha kuhifadhi maiti”alisema Mboya .
“Tumekuwa tukitenga na kwa kuwa ukarabati ulitakiwa uwe
mkubwa ,tumeendelea kutenga miaka yote na ilivyoingia serikali ya awamu ya tano
ikaingia na mkakati wa kuboresha vituo vya Afya na manispaa ya Moshi
tulifanikiwa kwa sababu ilikuwa kwenye mpango”alisema Mboya.
Alisema katika ukarabati huo serikali imetoa kiasi cha Sh
Mil 400 ikiwa ni mchango wake huku fedha nyingine zikitakiwa kutolewa na
Halmashauri hali iliyowalazimu kubadilisha matumizi ya fedha kwa baadhi ya
vifungu ili zikamalizie maeneo ambayo bado hayajakamilika katika kituo hicho.
“Kukamilika kwa kituo hichi kutawezesha wananchi wa maeneo
ya kata ya Bomambuzi ,Pasua ,Matindigani na Kaloleni waweze kupata huduma
ambayo ni ya kiwango na hasa tuilenga kwe nye eneo la wodi ya wazazi.”alisema
Mboya .
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Pasua ,Juma Raibu alisema
ukarabati wa vituo vya Afya ni mpngo mkakati wa taifa kwa ajili ya kuwasaidia
wananchi na kupunguza changamoto zilizokuwa zikiikabili sekta ya Afya nchini.
“Mimi kama Diwani nilipewa maelekezo kwa barua kwamba niunde
kamati mbalimbali za kuweza kusaidia ukarabati wa kituo hiki uweze kuendelea
,kamati ya kwanza niliambiwa niunde ya manunuzi,kamati ya mapokezi na kamati ya
ujenzi ili wazawa wa eneo hili wawe ni sehemu ya wasiamamizi wa mradi huu”alisema
Raibu.
Katika ziara hiyo Globu ya Jamii ilishuhudia wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwa wamoja katika kukagua maeneo mbalimbali
ya kituo hicho .
Mstahiki Meya ,Raymond Mboya(Chadema) akazungumzia hali hiyo na kuungwa mkono na Diwani
wa kata ya Kilimanjaro ,Priscus Tarimo wakieleza kuwa linapofika suala la
maendeleo itikadi za kisiasa huwekwa pembeni.
“Hii inaashiria Moshi tumekomaa ,nah ii inaashiria kwamba
kwa nini inaitwa Moshi ,kwamba baada ya uchaguzi kauli yetu ni maendeleo
,anayeleta siasa huwa hatumpia nafasi ,na ndio maana mimi kama Meya kwenye
baraza nawaambia tunaongea lugha ya maendeleo”alisema Mboya.
Mwisho
No comments:
Post a Comment