Leo tarehe 5 Januari, 2018 wakati wa Kipindi cha
Maswali na Majibu Bungeni Mwenyekiti wa Bunge, Mheshimiwa Najma Giga, (Mb)
alilazimika kusitisha kwa muda Kikao cha Bunge baada ya King’ora cha tahadhari
chenye kuashiria hatari kupiga kelele.
Hata hivyo, Wataalam wetu wamefuatilia na
kujiridhisha kuwa hakukuwa na tatizo la moto na hivyo Bunge lilirejea na
kuendelea na Kikao chake kama kawaida.
Aidha, hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa Waheshimiwa
Wabunge, Wafanyakazi wa Bunge wala Jengo la Ukumbi wa Bunge kufuatia taharuki
iliyosababishwa na King’ora hicho.
Imetolewa na:- Kitengo cha Mawasiliano
na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
No comments:
Post a Comment