HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 04, 2019

Special Olympics Tanzania yalia ukata michezo ya Dunia

Mkurugenzi wa Special Olympics, Charles Rays akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu kuomba udhamini wa safari ya kuelekea Abu Dhabi Falme za Kiarabu (UAE) kwenye michezo ya dunia inayotarajia kuanza Machi 14-21, katika michezo hiyo Special Olympics inahitaji shilingi milioni 45 kwa ajili ya kambi na usafiri, kulia kwa Rays ni Mjumbe wa Bodi, Makuburi Ally.

NA MWANDISHI WETU

TAASISI ya Michezo ya watu wenye ulemavu wa akili Tanzania, Special Olympics inahitaji shilingi milioni 45 kwa ajili ya kuisaidia timu ya Taifa inayotarajia kushiriki michezo ya Dunia itakayofanyika, Machi Abu Dhabi Falme za Kiarabu (UAE).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays alisema fedha hizo ni kwa ajili ya tiketi za kwenda na kurudi sambamba na kambi ya maandalizi kuelekea katika michezo hiyo.

Rays alisema kambi ya maandalizi kwa siku 14 inahitaji shilingi milioni 10,500,000 huku tiketi kwa ajili ya kwenda na kurudi Abu Dhabi ni shilingi milioni 34,527,600.

Aidha Rays alisema ili kufanikisha kushiriki katika michezo hiyo wameomba ridhaa ya Taasisi ya PRALENA Network Ltd ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa fedha hizo kupitia mfumo wa simu za mkononi.

Naye mwakilishi wa PRALENA, Thabit Said alisema ili kufanikisha upatikaji wa fedha hizo wametengeneza mifumo mbalimbali ambayo wadau watachangia fedha.

Said alisema mfumo huo utatumika kwa kila anayeguswa katika mitandao ya simu ya Tigopesa, M-Pesa na Airtel Money.

“Tunawaomba wadau katika jamii, kusaidia kupatikana kwa fedha hizo kupitia Tigopesa, M-Pesa na Airtel Money kupitia namba ya kampuni 123123 na kumbukumbu namba ni 60024833555,” alisema Said.

Said aliweka bayana kauli mbiu ya ufanikishwaji wa fedha hizo ni ‘Ushindi wao ni ushindi wetu’.

No comments:

Post a Comment

Pages