Ofisi ya CCM Upanga Magharibi baada ya kufanyiwa ukarabati na Diwani wa Kata hiyo.
Na Mwandishi Wetu
DIWANI wa Kata ya Upanga Magharibi (CCM), Adnan Kondo ametimiza ahadi yake ya ujenzi wa ofisi za Serikali ya Mtaa na Kata ya Upanga Magharibi kama alivyoahidi kipindi cha kampeni aliyotoa mwaka 2015.
Na Mwandishi Wetu
DIWANI wa Kata ya Upanga Magharibi (CCM), Adnan Kondo ametimiza ahadi yake ya ujenzi wa ofisi za Serikali ya Mtaa na Kata ya Upanga Magharibi kama alivyoahidi kipindi cha kampeni aliyotoa mwaka 2015.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kondo alisema ujenzi huo umekamilika hivi karibuni ambako amefanikisha hatua hiyo ya maendeleo kwa asilimia 98 huku asilimia iliyobaki imetokana na marafiki zake.
Kondo alisema gharama za ujenzi huo ni zaidi ya shilingi milioni 20 ambako alitoa wito kwa viongozi wenzake wa chama waliopata dhamana ya kuongoza kukijenga chama kwa hali na mali.
Alisema awali kabla ya kufanikisha ujenzi huo, miaka iliyopita katika ofisi hiyo lilikuwa banda ambalo lilikuwa halina hadhi ya CCM ndipo alipotekeleza ilani ya chama kwa vitendo.
"Nawaomba viongozi wenzangu tuliopata dhamana ya kuongoza tutekeleze kwa vitendo ili kukijenga chama kwa sababu asilimia kubwa ya wananchi wana imani kubwa na chama chao," alisema Kondo.
Aidha aliwataka wanachama wa Kata yake kuitumia vilivyo ofisi hiyo kwa shughuli za kimaendeleo kwani CCM ndio baba wa nchi hii.
No comments:
Post a Comment