HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 04, 2019

WABUNGE AMBAO HAWAJATIMIZA AHADI KWA WANANCHI WILAYANI MUFINDI HUKUMU YAO 2020

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Mufindi, Dickson Lutevele, aliyenyanua kofia akiwa kwenye moja ya picha ya maandalizi ya kumpoke mlezi wa chama hicho mkoa wa Iringa ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda. 

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi wilaya ya mufindi Dickson Lutevele amewataka wa wabunge wote wa wilaya ya Mufindi kuhakikisha wanatimiza ahadi zake zote alizoahidi ili kutatua Kero za wananchi na kuendelea kuaminika kwa wananchi waliowapa ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka mitano lasivyo hawatakuwa na nafasi ya kugombea tena ubunge kwenye Jimbo lake,CCM mpya inawataka wabunge wote kutimiza wajibu wao kwenye majimbo yao.

Hayo ameyasema wakati wa mahojiano na kituo cha radio kimojawapo cha mjini iringa wakati akijibu swali la mtangazaji aliyemhoji anawasimamiaje wabunge ambao hawatekelezi ahadi ambazo walikuwa wanaahidi kwa wananchi.

Lutevele alisema kuwa wananchi huwa wanakuwa na Imani na wagombea wa chama cha mapinduzi kwa zile ahadi ambazo huwa wanazinadi kwa wananchi na kuwapa matumaini ya kuleta maendeleo katika maeneo ambayo wanaishi lakini kuna baadhi ya wabunge hadi hii leo bado hawajamaliza kutekeleza ahadi ambazo wamezitoa kwa wananchi.

“Ndugu mtangazaji wewe pia umekuwa shaidi leo wasikilizaji kutoka wilaya ya Mufindi wakituma jumbe nyingi fupi za maandishi wakielezea kero ambazo wanazipota kwenye majimbo,kata na mitaa ambako huko kote viongozi wa kuchaguliwa na wananchi ndio wanaongoza,hivyo hata sisi kama chama tunazichukua na tuzifanyia kazi kwa kuwa chama cha mapinduzi ni taasisi kubwa  yenye kusimamia vizuri kanuni na katiba ya chama ili kutoa hadi na kuwalinda wapiga kura wake” alisema Lutevele

Lutevele alimalizia kwa kusema kuwa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi kinasaidia kuleta maendeleo kwa wananchi wa wilaya hiyo katika sekta ya afya,michezo,elimu na miundombinu na ndio sababu unaona kilakitu kimeboreshwa hapa Mufindi.

“Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John pombe magufuli kwa kusaidia kuboresha sekta ya afya na elimu wilayani Mufindi na wananchi wanaendelea kuwa na imani serikali yake maana tayari kuna vituo vya kuboreha vituo vya afya na kuzikarabati shule kongwe zote kama malangali na nyingine na vituo vya afya Ihongole,ifwagi na malangali" alisema Dickson lutevele maarufu kama villa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Wilaya ya mufindi

No comments:

Post a Comment

Pages