NA KENNETH NGELESI, MBEYA
KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya GGM kutoka Mkoani Geita
imeibuka washindi wa jumla katika maadhimisho ya usalama na afya mahali pa kazi
duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa tuzo na
vikombe mwakilishi wa kampuni ya GGM
Volentine Nahela alisema kuwa kuwa mbali na maadhimisho hayo
kusaidia kuonyesha mbinu za usalama mahali pa kazi lakini ilikuwa fursa
nzuri ya kujifunza kutoka kwa wengine.
Nahela alisema kuwa mbali na Mgodi huo kuibuka weashindi lakini
pia wamekuwa wakitoa mafunzo ya ya namna ya kukabilina na majanga migodini kwa
wachimbaji wadogo katika Mkoa huo wa Geita.
Akitoa taarifa ya matukio na majanga Nehela alisema kuwa GGM
wamekuwa makini na kwamba mwaka ulipo ita hakuna hata tukio moja lilitokea na
kuadhiri wafanyakazi wa mgodi.
‘GGM tupo vizuri katika masuala ya afya na usalama kazini hata
hivi tunashukuru leo kwani hkuana mtumishi aliyekatwa hata uckucha, kuibuka washindi
wa jumla ya kupata tuzo na vikombe vitatu lakini pia tumekuwa tukitoa mafunzo
ya masuala ya Afya na usalama pa kazi kwa wachimbaji wadogo’ wadogo alisema
Nahela.
Kwa Upande wake Waziri wa waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu,
uratibu wa bunge, sera, kazi, ajira na watu wenye ulemavu, Jenesta Muhagama
alipongeza kampuni hiyo kwa kufuata maagizo yalitolewa na Serikali wakati wa
maonmyesho kama hayo Mkoni iringi huku akiwataka wajiri kote nchini kuzingatia
sheria ya usalama na afya mahali pa kazi ili kuwalinda wafanyakazi kwa lengo la
kuongeza tija na uzalishaji.
Kwa upande wake waziri wa
madini, Dotto Biteko ameitaka migodi yote nchini na taasisi zilizo chini ya
wizara yake kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ya usalama na afya mahali pa kazi
ili kuepusha wafanyakazi wao na jamii kwa ujumla
No comments:
Post a Comment