Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amemuagiza
kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Juma Bwire, kuhakikisha anakamilisha
ujenzi wa nyumba za makazi ya askari wa Jeshi hilo unakamilika ndani ya kipindi
cha mwezi mmoja.
IGP Sirro amesema kuwa kukamilika kwa nyumba hizo
zilizotokana na fedha zilizotolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania Dk. John Magufuli, zitasaidia kukabilianana na changamoto ya makazi.
Aidha, IGP Sirro, ameipongeza kamati ya ulinzi na usalama ya
mkoa wa Iringa kwa kuendelea kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inazidi
kuimarika katika mkoa huo huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria
mkononi, ubakaji pamoja na kujihusisha na wizi wa kutumia pikipiki.
No comments:
Post a Comment