Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe jana wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi mkoani humo ambapo IGP Sirro, amezungumzia suala la kufuata sheria za nchi pamoja na kuwaonya wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya mauaji, ubakaji na wizi wa kutumia pikipiki.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP
Simon Sirro, akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole
Sendeka, wakati alipomtembelea ofisini kwake, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa
ziara ya kikazi yenye lengo la kufanya ukaguzi na kuzungumza na maofisa na
askari wa Jeshi hilo ikiwa pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za
makazi ya askari.
No comments:
Post a Comment