Mshambuliaji wa timu ya Simba SC ya Dar es Salaam, John Bocco
amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu Tanzania Bara
(TPL) msimu wa 2018/2019.
Bocco ametwaa tuzo
hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Donald Ngoma wa Azam FC na
Jaffari Kibaya wa Mtibwa Sugar SC alioingia nao fainali katika uchambuzi
uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya TPL inayotolewa
na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kwa
mwezi huo wa Machi, Simba ilicheza mechi tatu na kushinda zote, ambapo
Bocco alitoa mchango mkubwa kwa timu yake akifunga mabao manne na
kuifanya Simba iendelee kubaki nafasi ya tatu.
Kwa
upande wa Ngoma alikuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Azam FC
kwa mwezi huo, ambapo timu yake ilicheza mechi tatu ikishinda zote na
kuendelea kubaki nafasi ya pili, akifunga mabao manne.
Mshambuliaji
Kibaya alikuwa chachu ya mafanikio ya Mtibwa Sugar SC ambayo ilicheza
mechi nne, ikishinda tatu na kupoteza moja, huku ikipaa kutoka nafasi ya
12 hadi ya sita katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 20.
Kwa
kuibuka mchezaji bora, Bocco atazawadiwa sh. 1,000,000 (milioni moja)
na kombe (trophy) kutoka kwa wadhamini wa tuzo Biko Sports pamoja na
kisimbusi kutoka Azam TV ambao ndiyo wenye haki ya matangazo ya TPL.
Pia
Kamati ya Tuzo, imemchagua Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems kuwa
Kocha Bora wa Machi akiwashinda Kocha Mkuu wa Azam, Abdul Mingange na
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila.
Aussems
ameifanya Simba iendelee kung’ara katika ligi hiyo ambapo kwa mwezi huo
ilishinda michezo yote mitatu iliyocheza ikiwa nafasi ya tatu katika
msimamo wa ligi hiyo.
Kocha huyo pia atazawadiwa sh. 1,000,000 (milioni moja) na kombe (trophy) kutoka Biko Sports.
TFF
ina utaratibu wa kuwazadiwa wachezaji bora wa kila mwezi, huku pia
mwisho wa msimu kukiwa na tuzo mbalimbali zinazohusu ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment